Mshiriki wa mafunzo Hidaya Makame Juma akichangia mada katika Mafunzo ya Maendeleo Shirikishi katika Jamii(CBID)Ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya yaliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Afisa ufuatiliaji na Tathmini Madrasa Early Childhood Programme Zanzibar (MECP-Z) Awatif Ghalib Awadh akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafunzo ya Maendeleo Shirikishi katika Jamii(CBID)Ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya yaliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Mshiriki wa mafunzo Mudathir Sharif Khamis akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na faida wanayoipata katika Mafunzo ya Maendeleo Shirikishi katika Jamii(CBID)Ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya yaliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Washiriki mbalimbali waliohudhuria katika Mafunzo ya Maendeleo Shirikishi katika Jamii(CBID)Ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya yaliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
Mshiriki wa Mafunzo Abdalla Khamis Mjaka akichangia mada katika Mafunzo ya Maendeleo Shirikishi katika Jamii(CBID)Ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya yaliofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar.
***********************************
Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar
Jamii imetakiwa kuondokana na mtazamo potofu wakuwaona watu wenye ulemavu hawawezi kushirikishwa katika mambo mbali mbali ya kiuchumi na yanayoleta maendeleo.
Hayo ameyasema Afisa Ufatiliaji na Tathmini kutoka katika Mradi wa kushuhulikia haki za Walemavu (Madrasa Early Childhood Programme Zanzibar) Awatif Ghalib Awadh wakati akifungua mafunzo ya Maendeleo Jumuishi katika Jamii (CBID) Ngazi ya Kitaifa na Wilaya yaliyofanyika katika Ukumbi wa ZURA Mjini Unguja.
Amesema watu wenye ulemavu wanaonekanwa ni watu wasioweza shuguhuli yoyote ya kimaendeleo lakini katika ulimwengu wa sasa watu hao hufanya mambo mengi ya kuleta maendeleo katika jamii.
Aidha amefahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha watu wa Zanzibar kuwa na muamko juu ya haki za watu wenye ulemavu katika Nyanja zote za maisha ili kuzingatiwa hali zao .
Akifafanuwa zaid amesema mafunzo hayo pia yapo kwa ajili ya kuwatetea watu wenye ulemavu ili nao washirikishwe katika mambo mbali mbali ya kijamii ikiwemo kutoa maoni na kuonekanwa wanahaki ya kufanya hivyo.
Hata hivyo amesema kuwa kwasasa Zanzibar kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa watu wa aina hiyo kwani kila wanapojenga majengo huzingatia sehemu maalum za watu hao japo kuna baadhi ya majengo bado hayajakidhi mahitaji ya watu hao.
“kwa sasa Zanzibar kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa watu wenye ulemavu na majengo mengi hujegwa kwa kuzingatiwa mahitaji maalum ya watu hao japo kuna baadhi ya majengo bado hayakidhi haja zao.”amesema Awatif Ghalib.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano na Maendeleo katika Idara ya Watu Wenye Ulemavu Mmbaya Haji amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza Ufanisi katika kazi zao ili lengo la mafunzo liweze kutimia.
Vile vile amesema pia yatawasaidia katika kutoa elimu na kuondokana na dhana potofu inayowanyima haki zao na fursa wanazotaka kupatiwa.
Nae Mudathir sharif khamiss kutoka Jumuiya ya watu wenye Ulemavu wa ngozi Zanzibar amewaomba Baadhi ya watu wenye mtazamo tofauti kwa watu wenye ulemavu kuondoa zana hizo na kusema Mafunzo hayo yatarejesha hali ya Zanzibar ya kuondokana na tatizo la kutopata haki zao.