Meneja wa kanda ya Kusini Bi. Amina Yasini (TBS) akitoa mafun
zo kwa wadau wa bidhaa ya nafaka na mafuta ya kula wilayani Songea, Ruvuma.
Bi.Amina aliwafahamisha washiriki hao kuwa mafunzo hayo ni endelevu kwani TBS imeadhamiria kuwasaidia wadau kuhakikisha jamii inapata bidhaa bora na alishauri wazalishaji wasio na Leseni ya TBS kuanza utaratibu mara moja.
Afisa Tehama (TBS) Bi,Jesca Matemba akitoa elimu ya jinsi ya kutuma maombi TBS kupitia mfumo kwa wajasiriamali wa mafuta ya kula na nafaka katika eneo la majengo wilayani Songea.
Mkaguzi wa TBS, Bw. Barnabas Jacob akitoa elimu kuhusu madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania(TTCL) wilayani Songea, Ruvuma.
TBS kanda ya kusini imeendesha zoezi la usajili wa majengo ya chakula na vipodozi katika mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi na kubaini uwepo wa bidhaa hafifu za vipodozi na chakula sokoni zenye thamani ya shillingi millioni 12/= ambazo zimeteketezwa.
TBS inatoa wito kwa wauzaji na watumiaji wa bidhaa hizo kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na kuzingatia ukomo wa muda wa matumizi wa bidhaa husika.
Mkaguzi wa TBS Bw. Barnabas Jacob akitoa mafunzo kwa wasindikaji wajasiriamali wa nafaka na mafuta ya alizeti wa eneo la Majengo wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
Bw. Barnabas amewafundisha washiriki hao umuhimu wa viwango ,matakwa ya Viwango na namna gani viwango vinaweza kuwasaidia kuzalisha bidhaa bora ambazo zitaweza kuleta ushindani katika soko.