Home Biashara SERIKALI KUONGEZA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA MAZAO YA MAFUTA

SERIKALI KUONGEZA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA MAZAO YA MAFUTA

0


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa Wadau wa Alizeti uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida mkoani Singida tarehe 13 Juni 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe, na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe wakikagua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali mkoani Singida wakati wa mkutano wa Wadau wa Alizeti uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida mkoani Singida tarehe 13 Juni 2021.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe, na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe wakikagua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali mkoani Singida wakati wa mkutano wa Wadau wa Alizeti uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida mkoani Singida tarehe 13 Juni 2021.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Katikati), Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Binilith Mahenge (Kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa Alizeti uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida mkoani Singida tarehe 13 Juni 2021.

KAtibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akiwatambulisha washiriki wa mkutano wa Wadau wa Alizeti uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida mkoani Singida tarehe 13 Juni 2021.
 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Singida

Katika
mwaka 2021/2022 Serikali imeongeza bajeti ya Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI)
kutoka Shilingi bilioni 7.35 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 11.63 mwaka
2021/2022.

Vilevile,
bajeti ya Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA) kutoka bilioni 5.42 mwaka 2020/2021
hadi Shilingi bilioni 10.58 mwaka 2021/2022 ili kuongeza upatikanaji wa mbegu
bora zikiwemo mbegu za mazao ya mafuta.

Waziri
wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 13 Juni 2021 wakati
akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa Wadau wa Alizeti
uliofanyika katika ukumbi wa Caatholic Social Hall uliopo Manispaa ya Singida
mkoani Singida.

Prof Mkenda amesema
kuwa
Wizara ya
Kilimo itaendelea kuhamasisha uanzishaji wa mashamba ya pamoja (block
farming
) katika mikoa inayozalisha mazao ya mafuta kwa lengo la kurahisisha
utoaji wa huduma ikiwemo mbegu bora, mbolea, viuatilifu na zana bora za kilimo
pamoja na mafunzo ya kilimo bora kwa wakulima. Aidha, Serikali itaimarisha
kilimo cha mkataba kwa mazao ya mafuta kwa lengo la kuwa na uhakika wa masoko.

Serikali itaendelea kuboresha
mazingira ya uwekezaji na kuondoa vikwazo vya kisera na kisheria ili kuhamasisha
uwekezaji. Maeneo ambayo tumeanza kuyafanyia kazi ni mfumo wa upatikanaji wa
mitaji katika sekta ya kilimo na masuala ya kikodi kwenye mazao ya mafuta”
Amekaririwa Mhe Mkenda

 

Vilevile ameongeza kuwa katika kukabiliana na
uongezaji Tija na Uzalishaji serikali itaendelea kuimarisha huduma za ugani kwa
kuwapatia vyombo ya usafiri maafisa ugani ikiwemo kununua pikipiki 1,500, vifaa
maalum vya kupimia udongo (Soil Test Kits), visanduku vya ugani (Extention
Kits
), simu janja na kuwezesha  
uanzishaji
wa mashamba ya mfano kwa kila afisa ugani na kutoa mafunzo rejea.

“Huduma
hizo zitawezeshwa kwa kuwa Wizara imeongeza bajeti ya Kuimairisha huduma za
ugani kutoka Shilingi milioni 603 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 11.5
mwaka 2021/2022. Katika utekelezaji wa mpango huo, Wizara imechagua Mikoa
mitatu ya Kielelezo ambayo ni
Singida, Dodoma na Simiyu yenye fursa kubwa ya kuzalisha mazao ya mafuta
hususan alizeti na pamba” Amesema Prof Mkenda

Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda
amesema kuwa serikali ilikuwa ikitekeleza
Mkakati wa Kuendeleza Zao la
Alizeti kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020.

Ameyataja malengo mahsusi
yaliyoainishwa kwenye Mkakati huo ni pamoja na kuimarisha utafiti wa mbegu bora
na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya alizeti. Baadhi ya matokeo
yaliyopatikana ni
pamoja
na Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imesafisha (purification) mbegu bora ya alizeti aina
ya Record ili kuongeza uzalishaji na tija.

Mikakati mingine ni serikali kuidhinisha
matumizi ya mbegu bora 11 ambazo ni TARI-ILO2019, TARI-NA2019, Aguara4, Aguara6,
Hysun33, Supersun64, Supersun66, Michel, Ancilla, Archeo na Soleado, Serikali
imeendelea kuchambua mifumo ya kikodi katika tasnia ya mafuta. Katika eneo hili
hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza tozo za mafuta ghafi yanayoingizwa
kutoka nje ya nchi kutoka asilimia
10
hadi 25 na mafuta yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na cha mwisho (semi-refined and refined) kutoka 25 hadi
35 kwa mwaka ili kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya mafuta na
uchakataji wa mazao hayo ndani ya nchi.

Mafanikio mengine ni Kuondoa Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) kwenye mitambo ya kusindika na kuchuja mazao ya mafuta (Solvent Extraction Machine) ikiwemo
alizeti na kupunguza tozo zitokanazo na Ushuru wa Mazao (Crop cess) kutoka asilimia 5 hadi 3.

Kwa upande wa alizeti Waziri Mkenda amesema
kuwa serikali imeanza kuhuisha mkakati wa alizeti uliopita kwa kuwashirikisha
wadau katika mnyororo wa thamani ili kwa pamoja tubainishe changamoto zilizopo
na kuzipatia ufumbuzi.

Uzalishaji wa alizeti duniani umeongezeka kutoka tani milioni 44.3 mwaka
2015 hadi tani milioni 51.9 mwaka 2019. Katika mwaka 2019/2020 uzalishaji wa
alizeti nchini umefikia tani 649,437 ikilinganishwa na tani 561,297 za mwaka
2018/2019 na michikichi umeongezeka kutoka tani 42,176 hadi 42,386.