Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifungua semina ya wahariri wa vyombo vya Habari na waandishi wa habari iliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) inayofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM leo Jumamosi Juni 12,2021.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifungua semina ya wahariri wa vyombo vya Habari na waandishi wa habari iliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) inayofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM leo Jumamosi Juni 12,2021.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye akitoa ukaribisho kwa Waziri, Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)na washiriki wa semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Prof. Busagala akizungumza katika semina hiyo kuhusu Jukumu la (TAEC) kwa Taifa na jamii kwa ujumla katika kuhakiki usalama wa Mionzi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Prof.Lazaro Busagala akizungumza katika semina hiyo kuhusu Jukumu la (TAEC) kwa Taifa na jamii kwa ujumla katika kuhakiki usalama wa Mionzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za ATOMIKI (TAEC) Prof. Lazaro Busagala akizungumza jambo katika mkutano huo kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Bw. Peter Ngamilo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada zinzowasilishwa na wataalam kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)
Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam Tume ya Unguvu za Atomiki (TAEC), Dkt. Wilbroard Muhogora akiwasilisha mada kuhusu mionzi.
Mtafiti Mwandamizi Sayansi ya Nyukilia Alex Pius Muhulo akiwasilisha mada kuhusu mionzi katika matibabu na utafiti wa magonjwa.
Mhariri Mkuu wa Channel Ten Bi.Kissa Mwaipyana (Kushoto) akiwa pamoja na Mhariri wa Times Fm Bi.Taus Mboye wakifuatilia mada katika semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM leo Juni 12,2021.
Mwandishi wa Fullshangweblog Bw.Emmanuel Mbatilo pamoja na washiriki wengine wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalam kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC).
……………………………………………..
Teknolojia ya Nyuklia ni teknolojia mtambuka kwakua inatumika katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Afya, Kilimo Ujenzi, Maji , Viwanda, Barabara na Madini ambapo katika sekta ya afya hutumika kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Ameyasema hayo leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akifungua mafunzo ya Kitaifa kwa wahariri na Waandishi wa Habari Juu ya uelewa na Udhibiti na Matumizi Salama ya mionzi nchini yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza katika mafunzo hayo,Prof.Ndalichako amesema kupitia mafunzo hayo yataweza kuwajengea uelewa wahariri na waandishi wa habari kuhusu shughuli za Atomic na kuondoa dhana hasi iliyojhengea kwenye jamii.
“Kufuatia Mafunzo haya tunaimani kwamba itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhara kwa wananchi na mazingira kupitia matumizi ya mionzi isiyo salama kwakuwa waandishi wa habari na wahariri ni kiungo muhimu katika jamii kufikisha taarifa na kuijengea jamii uelewa kuhusu jambo fulani”. Amesema Prof.Ndalichako.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Prof.Lazaro Busagala amesema kuwa mafunzo haya yanaweza kusaidia kuondoa zana potofu katika jamii kwani kumekuwa na uelewa mhafifu kuhusu matumizi ya mionzi.
Amesema mafunzo haya ni endelevu na yatawafikia makundi mbalimbali katika jamii lengo likiwa jamii nzima ielewe matumizi sahihi ya mionzi kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema kuwa Chuo hicho ni mdau mkubwa wa masuala ya nguvu za atomiki ikiwemo chuo hicho kuwa na kozi maalumu kuhusu masuala ya nguvu za atomiki.
“Kwa mwaka wa masomo 2020/2021 Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimedahili wanafunzi 60 wanaosoma kozi inayohusiana na nguvu za atomiki huku kukiwepo na wanafunzi 7 wanaosomea shahada ya umahiri kuhusu masuala ya nguvu za atomiki”. Amesema Prof.Anangisye.