Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo, akizungumza na wadau wa mazingira katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnat Chaggu akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Mazingira (TEEA) Prof.Hussein Sosovere katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Mazingira (TEEA) Prof.Hussein Sosovere akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa mazingira wakifuatilia Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC) kuhakikisha Viwanda vyote vilivyowekezwa hapa nchini vinafanyiwa tathimini ya Mazingira.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) ambapo amesema kuwa Viwanda ambavyo bado havijafanyiwa tathimini ya Mazingira kufanyiwa hivyo mara moja.
Aidha amemtaka mkurungenzi wa NEMC kutoa tangazo maalumu kwa wawekezaji wote wanaposajili miradi mbalimbali kuhakikishe wanaanza na mchakato wa tathimini ya Mazingira huku akipiga marufuku kwa wawekezaji hao kuwatumikisha wataalamu bila kuwalipa.
Amesema wataalamu zaidi ya 1,000 Wamepatiwa usajili ambao unawawezesha kufanya tathimini ya athari za mazingira lakini wataalamu 250 pekee ambao ni sawa na asilimia 25% ya wote waliosajiliwa ndio wanafanyazi.
“Hata hapa kwenye mkutano nimeangalia hao wataalamu 250 waliohai kazini wengi wao hawajahuhudhulia mkutano huu ambapo watakosa fursa ya kujadili kanuni mpya za mazingira,kupitia mfumo mpya wa kimtandao wa kusajili vyeti vya mazingira kwa wahitaji kwahiyo wachache waliohudhilia watapata manufaa makubwa”Alisema Jafo.
Katika hatua nyingine Jafo amewaagiza wataalamu wa Mazingira kutumia Taaluma zao kuangalia njia bora ya kudhibiti athari ya madini ya zebaki ili kuepuka madhara yanaweza kujitokeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Mazingira (TEEA) Prof.Hussein Sosovere amesema kuna tathimini 5,000 zimeandikishwa lakini tathimini 55 pekee ndio zimepatiwa vyeti,hivyo inaonyesha wazi jinsi wataalamu wa mazingira wanaweza kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kuhakikisha Shughuli za maendeleo haziharibu mazingira.
Nae Mkurugenzi mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Gwamaka amesema kuwa tangu kuanza kwa usajili kwa njia ya mtandao imesaidia kuondoa ucheleweshwaji usiokuwa na ulazima pia imesaidia kuondoka watu wanaojiita wasaidizi elekezezi maarufu kama Makanjanja, wakati hawajasajiliwa na mamlaka husika.
Hata hivyo wawekezaji wametakiwa kuzingatia tathimini ya Mazingira kabla ya kuanzisha miradi yao hapa nchini.