UNAPOPITA kila mahali kwa sasa ndani ya Manispaa ya Singida
stori kubwa ya kimjini mjini ni juu ya uzinduzi utakaofanyika kesho wa
RESTAURANT ya kisasa na yenye hadhi ya kipekee mkoani Singida maarufu “NEXT
ROOM.”
Sio rahisi kupotea kiwanja hicho KIPYA kipo mjini kabisa
nyuma ya Ofisi za Tanesco za Mkoa Mtaa wa Ipembe ni njiani kabisa, wanaotoka njia ya
Jineri ukikunja tu kona ya Benki ya NBC kuingia sokoni unakutana na ‘Next Room’.
“Restaurant na Baa” hiyo ambayo wadau wengi
wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu sasa uzinduzi wake ni kesho Jumamosi, lakini mpaka
muda huu ninapoandika ishu hii tayari kuna watu wameshajisajili na wapo counter
pale site wanapasha.
Tofauti na maeneo mengine, hawa jamaa ‘Next Room’
wamejipanga vilivyo sana kwenye masuala yote ya vyakula kuanzia breakfast lunch na
dinner, jamaa wameamua kuajiri mashefu wale wanaotengenezaga misosi ya hotel za
Nyota Tano, full kufunika!
Ishu ya VINYWAJI ndio kabisaa usipime! vyote vyote vipo na mdau
wakati anakula na kunywa atasindikizwa na SCREEN kubwa sana ambazo zimetapakaa
kila mahali kuwanasa vizuri wale wapenzi Liverpool, Manchester United,
Arsenal, Wekundu na sisi wa njanooo.
Kiukweli pako fresh! Mandhari yake imetulia kama unavyoona kwenye
picha hapo chini na unaruhusiwa hata kutoka kifamilia mana hakuna mbwembwe
nyiiingi sana za mziki wa juu hapana! kuna mziki wa kiwango kiasi chake, na
uzinduzi wa kesho utasindikizwa na ‘Live Band kutoka pande za Kigoma.’
Muonekano wa baadhi ya viti ndani ya Restaurant hiyo.
Mandhari ya kuvutia nje ya Restaurant hiyo.
Mandhari ya kuvutia nje ya Restaurant hiyo.
Muonekano wa moja ya Kaunta zake za ndani.
Muonekano wa baadhi ya viti ndani ya Restaurant hiyo.