Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amekabidhi gari la wagonjwa kwa uongozi wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya makabidhiano yaliyoshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera.
Masache amesema gari hilo lisaidie changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Chunya.
Akipokea gari hilo kutoka serikalini Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka Simon Mayeka amesema gari hilo litumike kama ilivyokusudiwa.
Hafla hiyo imeshuhudiwa pia na Mkurugenzi wa Wilaya ya Chunya Sophia Kumbuli.