Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6,2021 jijini Dodoma kuhusiana na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha mikopo minne yenye masharti nafuu yenye jumla ya dola za Marekani bilioni 1.017 (sawa na shilingi trilioni 2.3391) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wa Wizra wakifatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ,wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6,2021 jijini Dodoma kuhusiana na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha mikopo minne yenye masharti nafuu yenye jumla ya dola za Marekani bilioni 1.017 (sawa na shilingi trilioni 2.3391) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimasikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza nao kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwemo mkopo wa Benki ya Dunia, Deni la Taifa, makusanyo na akiba ya fedha za kigeni, leo Juni 6,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
BODI ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imetoa mkopo wa Masharti nafuu kwa Serikali ya Tanzania jumla ya dola za kimarekani bilioni 1.017 Sawa na shilingi trilioni 2.3391 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hayo yameelezwa leo Juni 6,2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Dkt.Mwigulu amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia iliidhinisha mikopo mitatu ya masharti nafuu yenye jumla ya dola za Kimarekani milioni 875 Sawa na shilingi Trioni 2.0125 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji miradi ya Maendeleo nchini.
“Tarehe 3 Juni 2021 bodi hiyo iliidinisha mkopo mwingine wenye thamani ya dola za Marekani milioni 142 Sawa na shilingi bilioni 326.6 na kufanya jumla ya mikopo yenye mashariti nafuu iliyoidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia minne ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 1.017 Sawa na sh.2.3391.
” Miradi iliyopata idhini ya bodi ni Mradi wa Roads to Inclusion and Socio -economic Opprtunities (RISE),wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 300,mradi wa Higher Education for Economic Transformation Project (HEET) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 425,mradi wa Digital Tanzania Project (DTP) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 250 na mradi wa Zanzibar Energy Sector Transformation and Access Project wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 142″ ameeleza Dk.Mwigulu.
Dk.Mwigulu ameitaja miradi mingini kuwa ni mradi wa RISE ambao utasaidia kuboresha barabara za vijijini na kutoa fursa za ajira takribani ajira 35,000 kwa wananchi waliopo katika vijiji nufaika pamoja na kujenga uwezo wa usimamizi endelevu wa Barbara za vijijini kwa kuhusisha njia shirikishi za jamii.
“Mradi huu utahusisha ujenzi wa jumla ya kilometa 535 kwa kiwango cha lami katika wilaya sita za mikoa ya Iringa,Lindi,Geita,na Tanga na ukarabati wa maeneo korofi ya barabara za vijijini nchi mzima” amesema Dk Mwigulu.
“Kuna mradi wa DTP utasaidi kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa Inaneti na kuboresha huduma za Umma kwa kutumia digitali kwa kustawisha ekologia ya kidigitali nchini,kuhakikisha uunganishaji wa kidigitali kwa watanzania wote na kuboresha jukwaa la huduma za kidigitali.
” Mradi wa ZESTA utasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora nanza uhakika za umeme visiwani Zanzibar ikiwa ni pamoja nankujenga mitambo ya nguvu ya jua na msongo wa kV 132 wa kusafirishia umeme katika visiwa hivyo.
“Vile vile mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya mradi wa Boosting Inclusive Growth for Zanzibar (BIG-Z),unategemewa kuwasilishwa katika katika vikao vya bodi ya Benki hiyo tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kupata idhini,mradi huu utasaidia kuboresha miundombinu ya mijini katika miji ya Unguja na Pemba kwa kujenga na kuboresha barabara za lami ,mifumo ya maji taka ,mifereji ya maji ya mafuriko ,maeneo ya uthibiti mjini Unguja na Pemba ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na uwekezaji na kukuza utalii katika visiwa vya Zanzibar” amefafanua Dk.Mwigulu.
Kuhusu deni la taifa amesema deni la taifa,likijumuisha la sekta binafsi hadi mwisho wa Aprili 2021 ni dola za Marekani milioni 31,986.7 kati ya deni hilo deni la nje ni dola za Kimarekani milioni 24,477.6 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1.
”Deni la Taifa alisema kuwa mpaka sasa deni la Serikali ni dola za Marekani milioni 26,416.8 (sawa na Tshs 60.719.01 bilioni) ikijumuisha deni la nje dola za Marekani milioni 18,907.7 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1 (sawa na sh. bilioni 17,259.9 na kwamba deni hilo ni himilivu.” ameeleza Dk.Mwigulu.
Waziri Nchemba ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia, Menejimenti ya Benki ya Dunia Ofisi ya Tanzania, pamoja na Watumishi wote wa Serikali walioshiriki katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.