Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanawake zaidi ya 10,000 wa makundi mbalimbali wanatarajia kushiriki Mkutano na Rais Samia Suluhu Hassan, Juni 8, mwaka huu utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Juni 6,2021 kuhusu wanawake zaidi ya 10,000 wa makundi mbalimbali wanatarajia kushiriki Mkutano na Rais Samia Suluhu Hassan, Juni 8, mwaka huu utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisoma baadhi ya vitabu vilivyopo katika Ofisini kwake leo Juni 6,2021 mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano wa wanawake na Rais Samia Suluhu Hassan, Juni 8, mwaka huu utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wanawake zaidi ya 10,000 Mkoa wa Dodoma makundi mbalimbali wanatarajiwa kukutana na Rais Samia Hassan Juni 8 mwaka huu katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Hayo yamesemwa leo Juni 6,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Mtaka amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya kina mama wa mikoa yote.
”Wakina mama kwa uwakilishi wao wa makundi mbalimbali kutoka wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki kwenye mkutano huo”amesema
Aidha ametaja makundi hayo ni pamoja na wabunge wanawake bila kujali uko chama gani, madiwani na makundi kama wajasiriamali, mama ntilie na kila aina ya kina mama watapata nafasi ya kuwakilishwa na wenzao.
Hata hivyo Mtaka amewakaribsha waandishi wa habari na kuwataka kufanya kazi naye kwa ushirikiano .