WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,akitoa neno wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la CARE International Tanzania pamoja na wageni waalikwa wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,akifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akizindua Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma..kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma..
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiwa na washiriki wa Maendeleo wakionyesha Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui
Meneja wa Mradi wa Ardhi yetu unaofadhiliwa na Serikali ya Denmark Daniel Katebalila,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma. leo June 4,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Ikiwa jamii ya kitanzania bado ikikabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira hali ambayo huchagizwa na wananchi kutokuwa na uelewa juu ya athari zitokanazo na uharibifu huo,Shirika la kimataifa la CARE limesema kuwa limekuja na mkakati kababe wa kutoa elimu kwa jamii na kuijengea uelewa wa utunzaji wa Mazingira na kuiweka Tanzania Salama kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa mwaka 2021-2026 .
Akizungumza leo Juni 4,2021 jijini Dodoma wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 -2026, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui amesema katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi shirika hilo limekuwa na program mahsusi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii kupunguza matumizi ya mkaa.
”Mkakati wetu ni kutoa elimu kwa jamii na kuijengea uelewa wa utunzaji wa Mazingira ili kuongoa mfumo wa Ikolojia kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na kuiweka Tanzania Salama kwa mwaka 2021-2026”amesema Bi.Haika .
Amesema kuwa Shughuli za binadamu Kama vile Kilimo,uchimbaji wa madini ,uchomaji mkaa na ufugaji ni vyanzo vikubwa ambavyo huharibu mazingira,jamii inapaswa kwenda na wakati kwa kufuga kisasa lakini pia kutumia nishati mbadala.
Bi.Haika amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuonyesha utayari katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kutokana na ongezeko la shughuli za kibinaadamu.
“Mabadiliko hayo yamesababisha kubadilika kwa misimu ya mvua ambako maeneo mengine zinanyesha juu ya wastani na chini ya wastani,” ameeleza.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Ardhi yetu unaofadhiliwa na Serikali ya Denmark Daniel Katebalila amesema kuwa mkakati huo utasaidia wanajamii kuwa na uelewa zaidi juu ya mabadiliko ya Tabianchi.
Awali Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo ametoa maagizo juu ya utekeleaji wa mpango huo kila taasisi kutoa elimu na kuimarisha mashirikiano baina na serikali pamoja na tafiti.
Maadhimisho ya Mazingira Duniani yanatarajia kuhitimishwa kesho Mei 5,2021 na Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais wa Tanzania ,Dkt.Philiph Mpango ambapo yanakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘’Tutumie Nishati Mbadala kuongoa mifumo ikolojia