Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi ,akizngumza na watumishi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) leo June 3,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mtandao THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa ,akizngumza na watumishi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) leo June 3,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na watumishi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) leo June 3,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa kutetea Haki za binadamu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kama ilivyo ainishwa katika katiba na ilani ya Chama cha Mapindizi (CCM) 2020/2025.
Akizungumza na watumishi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa kutetea haki za binadamu kwenye masuala ya kupigania haki za msingi.
“Tuko tayari kushirikiana na wadau ninyi muhimu kwenye masuala ya kupigania haki za wananchi tunajua kuwa mtakua na vipaumbele vyenu muhimu na serikali pia itakuwa na vipengele vyake ambavyo vinalenga kukuza haki za binadamu nakuleta maendeleo katika nchi yetu,
“Hayo yote ni matakwa ya ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kuwa serikaki imeahidi kuheshimu na kuzingatia haki za binadamu kwa mtu mmoja mmoja, makundi na makundi ili kujenga jamii yenye usawa,” alieleza kabudi
Aidha alisema Tanzania sio nchi yakufundishwa kupigiania haki za binadamu kwani ni suala ambalo lilianza tangu zamani sana na kila kitu kimeandikwa kwenye katiba.
Kwa Upande wake Mratibu wa Mtandao wa Onesmo Olengurumwa THRDC alisema serikali inatambua kuwa mfumo bora wa sheria ndio msingi wa kutekeleza matakwa ya katiba,Sera,na mpango wa nchi.
Alisema asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamiii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.
“Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya vizuri sana hapa nchini tunaomba serikali itambue mchango wa asasi hizo na kuongeza ushirikiano ili zziendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,” alisema
Olengurumwa aliihakikishia serikali kuwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati bila vipingamizi vyovyote.