Home Siasa SIMBA YALIPA KISASI KWA RUVU SHOOTING YAICHAPA 3-0 UWANJA WA CCM KIRUMBA...

SIMBA YALIPA KISASI KWA RUVU SHOOTING YAICHAPA 3-0 UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA

0
MABINGWA watetezi, Simba SC walipa kisasi kwa Ruvu Shooting baada ya kuichapa mabao 3-0 mchezo wa Ligi  Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa  Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao ya Simba yamefungwa na John Raphael Bocco dakika ya 18 na dakika  ya 88 kwa penalti baada ya kipa wa Ruvu, Abdallah Rashid kumuangusha winga Mghana, Bernard Morrison kwenye boksi.
Bao lingene limefungwa na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu kufunga bao la pili dakika ya 62.

Ruvu Shooting ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya wachezaji wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, beki wake, Juma Said Nyosso dakika ya 72 na kipa Abdallah Rashid dakika ya 87.

Kwa matokeo hayo  Simba SC imefikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya Yanga ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.