Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Aboubakar Kunenge akivishwa shafu na vijana wa skauti baada ya kuwasili katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Bagmoyo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kwenda kujitambulisha kwa watumishi na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na kuzungumza na wataalamu na wakuu wa idara.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Aboubakar Kunenge akiwasalimia baaadhi ya viongozi mbali mbali wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ambapo aliwasili kwa lengo la ziara maalumu ya kwasalimu.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Aboubakar Kungenge akiwa amenyanya zawadi maalumu ambayo amepatiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bagamoyo kwa ajili ya kukaribishwa rasmi , kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr Delphine Magera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere akiwa anatoa neno la shukrani wakati wa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kwenda kujitambulisha.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU,)
******************************
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mh. Aboubakar Kunenge amewataka na kuwaagiza wataalamu na watumishi wote wa halmashauriya Bagamoyo kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa weledi na kutumia vema ipasavyo ujuzi walionao katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika maeno yao ya kazi na kutumia fursa zilizopo katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kunenge ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika halmashauri ya Bagamoyo kwa lengo la kuweza kujitambulisha pamoja na kuzungumza na baadhi ya watumishi wakuu wa idara pamoja na wataalamu kwa lengo la kuweza kupeana maelekezo katika suala zima zima uwajibikaji.
Aidha kunenge katika kikao hicho amewakumbusha wataalamu kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati madhubuti katika suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuwez kuwaletea wananchi maendeleo.
“Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa awamu ya sita Mama Samia Samia Suluhu kwa kuweza kuniamini tena naa kunipanafasi ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani lakini lengo langu kubwa nimekuja kuwasalimia ili tuweze kuweka miapango madhubuti ambayo itasaidia katika kuleta chachu ya maendeleo katika maeneo yetu.”alisema Kunenge.
Aidha Kunenga aliwataka wataalamu mabali mbali kujenga tabia ya kufanya utafiti ambao utawasaidia katika kubaini fursa mbali mbali zilizopo katika maeneo yao kwa lengo la kuweza kuzitumia kikamilifu ili ziweze kuleta matokeo chanya na mafanikio katika maeneo ambayo wanayafanyia kazi.
Pia alibainisha kwmaba watumishi na waattalamu wanatakiwa kushirikiana bega kwa bega katika Nyanja mbali mbali na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo ilengo ikiwa ni kuweka mipango madhubuti ambyo itaweza kuzaa matunda katika siku za usoni na kwamba lengo la serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo.
Kadhalika Kunenge alisema kwamba lengo la serikali iliyopo madarakani ni serikali ya Chama cha mapinduzi (CCM) hivyo ni lazima itatekeleza Ilani ya Chama katika ni kuhakikisha inatumikia wananchi wananchi na kuzisikiliza kero na changamoto zao mbali mbali zinazowakabili.
“Kitu kikubwa ambacho nina kiomba kwa watumishi wote wa umma ni lazima kuweka mikakati ya kutekeleza ilani ya cahama cha mapinduzi kwa vitendo kwa serikali hii ndio inasimamiwa na CCM na kwamba ni lazima watumishi wote kw akipindi hiki inapaswa kchapa kazi kweli kweli kwa bidii ili tuweze kutumiza yale yote amabyo yameelekezwa katika Ilani ya Chama.
Katika hatua nyingine Kunenge aliongeza kwamba atahakikisha kwamba anashirikiana na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuuu wa wilaya wakurugenzi ili kuweza kufikia lengo ambalo limekusudiwa na serikali katika kuwatumikia wananchi pamoja na kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Awali kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo Zainabu Kawawa akisoma taarifa ya Wilaya hiyo alisema kwa sasa bado kuna changamoto mbali mbali amabzo zinatakiwa zifanyiwe kazi ikiwemo kukithiri kwa uwepo wa bandari bubu 19 amabzo zimekuwa zikitmika katika kufanyia biashra za magendo.
Aidha Kawawa aliongeza kwa sasa katika kukabiliana na changamoto hiyo wameshaanza kufanya misako na doria mbali mbali katika bahari ya hindi kwa lengo la kuwabaini wale wote ambao wanahusika na matukio mbali mbali ya kuharifu kupitiabandari hizo bubu.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere aliwahimiza watumihshi na wataalamu mbali mballi kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia wananchi naa kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa maslahi ya wananchi.