************************************
TBS imetoa mafunzo kwa wazalishaji, wauzaji, wasambazaji na wadau mbalimbali wa viungo mkoani Morogoro ambapo imewataka kuendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango ili kuweza kumlinda mtumiaji.
Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Bw.Hamisi Mwanasala amesema kuwa wajasiriamali wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo wameona ni vyema kuwapa mafunzo ili kuhakikisha wanazalisha na kuuza bidhaa zilizokidhi viwango.
“Ili tuendelee kukuza biashara zetu tunatakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na tuweze kuingia katika soko la ushindani na tuendele kuwa kwenye soko la ndani na nje”. Amesema Bw.Mwanasala.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yataweza kusaidia kuboresha bidhaa za wajasiliamali kwa kuongeza thamani ya bidhaa na ziweze kukubalika kwenye masoko ya ndani na nje.