***************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mkuu wa mkoa wa Arusha mstaafu Iddi Kimanta amemuomba Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kuhakikisha anakamilisha utekelezaji wa ujenzi wa hospitali za Wilaya ya Longido,Ngorongoro pamoja na ujenzi wa Ofisi ya kisasa ya Jiji la Arusha.
Kimanta alitoa ombi hilo wakati wa hafla ya kumuaga na kumpokea Mkuu wa mkoa mpya John Mongela ambapo alisema kuwa Jiji la Arusha halina Ofisi ya kutosha kukidhi mahitaji yake jambo linalopekea mafaili ya Jiji kutembezwa kutoka Jiji kupelekwa Njiro,kutoka Jiji kupelekwa Kilombero
“Nilitamani kuona jengo kubwa jiji lenye hadhi ya mkoa wa Arusha Geneva ya Afrika hivyo nakuomba ujenzi tayari upo kwenye mpango simamia iweze kukamilika kwa manufaa ya jiji letu,mkoa na Taifa kwa ujumla,” Alisema Kimanta.
Aidha Kimanta, alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufikisha umri wa miaka 62 na kustafu salama ,kwani ametumika serikalini kwa miaka 39 ambapo amekuwa kiongozi wa kawaida kwa Miaka 30 na kiongozi kwa Mika 9
Alisema kuwa Jambo ambalo atalikumbuka kwa Arusha zaidi ni ushirikiano,upendo alioupata kutoka kwa watendaji kazi wenzake ambao alitumika pamoja na kumuhakikishia Mongela anayechukua nafasi yake kuwa yupo mikono salama
”Kazi ya kuwatumikia wananchi siyo rahisi inahitaji kumtanguliza Mungu wakati huu ninapostaafu ndipo ninapojua kuwa nilibeba mzigo mzito nilikuwa silali kabisa lakini Sasa nalala,wengine wananionea huruma sasa mnanipa pole wakati mnatakiwa kunipongeza”alisema Kimanta.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa kwa kuwa Rais Samia Suluhu ameweza kumwamwini na kumkabidhi mkoa wa Arusha anahidi uongozi shirikishi ikiwa Ni pamoja na kuwatumikia wananchi sawa sawa na alichokula kiapo.