Kwa niaba ya mshindi wa kwanza wa gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni ya Bonge la Mpango – Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma, ambaye ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni hii katika picha Jacqline Kihongozi akifungua gari hilo(Lifan) baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto Baragomwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Tawi la NMB Chamwino. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati- Nsolo Mlozi.
Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto Baragomwa akimkabidhi kadi ya gari aina ya Tata Lifan alimaarufu Kirikuu ,Jacqline Kihongozi, aliyepokea kwa niaba ya mshindi wa kampeni ya bonge la Mpango inayoendeshwa na NMB, Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma ambaye ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni hii. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati- Nsolo Mlozi.
…………………………………….
Hadija Iddi mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma amekuwa mshindi wa kwanza kuzawadiwa gari aina ya TATA Ace
maarufu kama Kirikuu yenye thamani ya sh. Millioni 25, baada ya kushinda katika kampeni ya Bonge la Mpango
inayoendeshwa na Benki ya NMB.
Akimkabidhi gari hiyo Bi. Hadija, Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa alisema,
Bonge la Mpango inaendelea nchini kote na zawadi mbakimbali zinaendelea kutolewa, hivyo wateja wanaendelee
kufungua akaunti na kuweka hela kuanzia sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB ili waweze kuingia katika
kinyanganyiro cha Zawadi mbalimbali zinazotolewa katika kampeni hii ikiwemo, gari ya kifahari aina ya Toyota
Fortuner mpya yenye thamani ya Sh.169 milioni, gari ya miguu mitatu(Lifan) na pesa taslimu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Hadija aliishukuru benki ya NMB na kusema kuwa gari hilo
litamsaidia katika shughuli zake za kujiongezea kipato lakini pia akawashauri watanzania kuwekeza katika benki
hiyo kwani ndiyo benki bora Tanzania na pia inawajali wateja wake kwani amekuwa shahidi.
"Nimeamini kuwa yanayozungumzwa ni kweli,nimekabidhiwa gari mpya,nimepewa ufunguo na Kadi ya gari
vikiwa kamili kabisa, kweli NMB ndiyo mpango mzima,"alisema Hadija.
Wakati huo huo, Meneja wa NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania walichezesha droo nyingine kwa ajili ya kuwapata washindi wa wiki, ambapo watu
mbalimbali walipata fedha taslimu wakati na Henry Semwanza kutoka Chamwino and Faustine Nyawigrika wa
Biharamulo wakijishindia gari ya mataili matatu (Lifan) mpya kila mmoja.
Hadi sasa, NMB imetoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 145 zikiwemo; fedha taslimu, pikipiki za miguu
mitatu aina ya LIFAN na Tata Ace kwa washindi wa Bonge la Mpango.