Diwani wa Kata ya Msasani, Luca Neghesti, kulia leo hii amepokea mchango wa mabati 300 kutoka taasisi ya Karimjee-Jivanjee Foundation.
Mabati hayo yatatumika kuezeka baadhi ya madarasa katika shule za Kata ya Msasani ambazo zinakumbwa na adha ya maji kuvuja kipindi cha mvua, kwa lengo la kuwatengezea mazingira bora ya elimu wanafunzi wa kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam kama ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 inavyoelekeza.
Akizungumza katika shule ya msingi Msasani diwani huyo ameishukuru taasisi ya Karimjee-Jivanjee Foundation kwa kutoa msaada huo kwa sababu utasaidia kukwamua pakubwa maendeleo ya elimu katika kata ya Msasani.
Amesema Bahati mbaya Shule zetu ziko kwenye kata nyeti, watu wengi wanadhani shule hizo hazina matatizo lakini changamoto huwa hazikosekani, Msaada huo utapungumza baadhi ya changamoto katika shule zenye uhaba wa vyumba vya madarasa na vyumba vinavyovuja wakati wa mvua,
Diwani Luca Neghesti amesema mabati hayo yatagawanywa katika shule mbalimbali kwenye kata hiyo kulingana na mahitaji na amewaomba wadau wengine kuiga mfano wa taasisi ya Karimjee-Jivanjee Foundation ili nao waweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya elimu.
Ameipongeza serikali kwa kujenga madarasa mapya ambayo pia yamesaidia kuongeza kupunguza uhaba wa vyumba na kuongeza ubora wa elimu katika kata hiyo na nchini kote.
“Tutaendelea Kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Sukuhu Hassan katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kuboresha elimu nchini,”.Amemaliza Luca Neghesti