Kaimu Katibu Mtendaji Sekretariaeti ya Bonde la Mto Songwe, Mhandisi Gabriel Kalinga akitoa maelezo kuhusu Mto Songwe kwa wajumbe ya Bodi ya Maji ya Taifa walipokuwa ziarani kujionea shughuli usimamizi wa rasilimali za maji katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Kaimu Katibu Mtendaji Sekretariaeti ya Bonde la Mto Songwe, Mhandisi Gabriel Kalinga akitoa maelezo kuhusu Mto Songwe kwa wajumbe ya Bodi ya Maji ya Taifa walipokuwa ziarani kujionea shughuli usimamizi wa rasilimali za maji katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Wajumbe ya Bodi ya Maji ya Taifa kwenye eneo la Katumba-Songwe ambalo ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na shughuli za rasilimali za maji kupitia Programu ya Kuendeleza BonWajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa wakiwa kwenye chanzo cha maji cha Nyibuko kukagua shughuli za rasilimali za maji katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.de la Mto Songwe katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa wakiwa kwenye chanzo cha maji cha Nyibuko kukagua shughuli za rasilimali za maji katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.
Afisa Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa, Mhandisi Elice Englebert akitoa taarifa ya majukumu ya bonde kwa wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa katika Makao Makuu ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa yaliyopo wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
Kituo cha kupima wingi na usawa wa maji kwenye mto Kiwira kinachosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
…………………………………………………………….
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Maji wametembelea Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe na kujionea utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawi katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Programu hiyo inalenga utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kingo za Mto Songwe kwa awamu tatu zinazohusisha upembuzi yakinifu, usanifu na utekelezaji kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili ili kuimarisha mahusiano ya ujirani mwema na kuzingatia misingi ya umoja wa Afrika.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa, Dkt. Halima Kiwango amesema Wizara ya Maji inafanya kazi nzuri kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa kwa mujibu wa Sheria ya Maji Na. 5 ya Mwaka 2019, akisisitiza kuwa ujenzi wa miradi ya maji ni lazima uende sanjari na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuweza kukidhi mahitaji makubwa ya huduma ya maji kwa wananchi.
Akisema kuwa kazi kubwa imefanyika, ila Bodi za Maji za Mabonde ziongeze jitihada zaidi na kumaliza changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji na kuliondoloea taifa hatari ya kuingia kwenye hali ya uhaba wa maji.
Aidha, wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa wametembelea na kujionea shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji zinazofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa kwa kukagua chanzo cha maji cha Nyibuko pamoja na kituo cha kupima wingi na usawa wa maji kwenye mto Kiwira katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya na kuridhishwa na maendeleo yake.
Wajumbe hao wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika na kusababisha wingi na ubora wa maji kwenye chanzo cha maji cha Nyibuko ambacho chemchemi yake inapeleka maji yake kwenye mto Nyibuko kuongezeka, ambao unamwaga maji yake kwenye mto Kiwira.