Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya National Democratic Institute (NDI) nchini Tanzania, Bi, Sandy Quimbaya akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza leo jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika ili kujadili namna ambavyo ORPP inaweza kushirikiana na NDI kutoa elimu ya kukuza Demokrasia katika nyanja jumuishi ya ushiriki wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika siasa. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango,Ufuatiliaji, Tathimini,Bw. Eliuther Mazome na Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapeyo. Afisa Ufuatiliaji, Tathmini na Mafunzo ambaye pia ni Afisa Programu wa Taasisi ya National Democratic (NDI), Bi. Lyidia Christian akichangia hoja wakati wa kikao baina yao leo jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika ili kujadili namna ambavyo NDIinaweza kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) kutoa elimu ya kukuza Demokrasia katika nyanja jumuishi ya ushiriki wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika siasa.
Baadhi ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakifuatilia hoja kuhusu namna ya mashirikiano baina ya ORPP na Taasisi ya National Democratic (NDI) katika kutoa elimu ya kukuza Demokrasia katika nyanja jumuishi ya ushiriki wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika siasa. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Eleuther Mazome, Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapeyo, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Afisa Sheria, Bi. Grace Mushi.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa(ARPP), Sisty Nyahoza akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya National Democratic Institute (NDI) nchini Tanzania, Bi, Sandy Quimbaya (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao baina yao leo jijini Dodoma.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza (wapili kushoto) akiwa latika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya National Democratic Institute (NDI) nchini Tanzania, Bi, Sandy Quimbaya (wapili kulia) mara baada ya kumaliza kikao baina yao leo jijini Dodoma. (Picha na ORPP).