Home Mchanganyiko NJOREFA YAUNDA KAMATI NA KUZIINGIZA KAZINI PAPO HAPO NJOMBE

NJOREFA YAUNDA KAMATI NA KUZIINGIZA KAZINI PAPO HAPO NJOMBE

0

**********************************

Njombe

Siku moja baada ya uchaguzi wa njorefa kufanyika ,kamati tendaji ikiongozwa na mwenyekiti wa chama Cha mpira mkoa wa Njombe thobias Lingalangala imeunda kamati mbalimbali ambazo zitasimamia maendeleo ya mpira mkoan humo na kutoa onyo kwa ataezembea na kuonekana kikwazo katika jitihada za kukuza soka
Akitoa ufafanuzi wa kuharakisha uundwaji wa kamati na Aina ya Viongozi wasiotakiwa katika kipindi hiki Cha kunusuru soka la Njombe ambalo linazidi kudidimia kila iitwapo leo Lingalangala Amesema yeyote atakaeonesha kushindwa kuendana na Kasi yake ajiengue kabla hajaenguliwa na Kisha kutoa agizo la uwajibikaji.
Kuhusu kamati zilizoundwa na wajumbe wake , makamu mwenyekiti wa njorefa amesema zipo 5 na kuwataja wajumbe wake pamoja Viongozi wa kamati hiyo ambao papo hapo wameingia kazini.
Kamati ambazo zimeundwa ni ni Kamati ya fedha ambayo mwenyekiti wake ni Erasto Mpete ,Kamati ya Ligi na Mashindano ambaye mwenyekiti wake Lusubilo Mwakafuje,Kamati ya Ufundi mwenyekiti akiwa ni Meshack Mnyawasa ,Huku Kamati Vifaa mwenyekiti wake akiwa ni Musa Muhagama 
Kamati zimeanza utekelezaji wa maagizo ikiwemo kuvitambua Tena vilabu vya ngaz zote vya mkoa wa Njombe,maandalizi ya ujenzi w ofisi na kuirejeshea makali Tena njombe mji ili kurejea kigi kuu misimu ijayo.