Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akisaini kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini huku Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Lucy Saleko (kushoto) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mary Masanja ( kulia) wakishuhudia utiaji saini huo katika hafla hiyo iliyofanyika leo Jijini Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza kabla ya hafla ya utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji katika maeneo ya Uhifadhi nchini ambapo amesema kanuni hizo zinamruhusu Mwekezaji kumiliki eneo la Uhifadhi kwa miaka isiyopungua miaka 25
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akizungumza kabla ya hafla ya Utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimakakati katika maeneo ya Uhifadhi ambapo amesema Kanuni hizo zitasaidia kuongeza Wawekezaji katika sekta ya Utalii nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jen ( Mstaafu) Hamisi Semfuko akizungumza kabla ya hafla ya utiaji saini Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi ambapo amesema anatarajia Uwekezaji huo utaongeza mapato Serikalini kwa vile unalenga Wawekezaji wakubwa
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt.Maurus Msuha ( kulia) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Lucy Saleko wakimfutilia Waziri wa Maliasili na Utalii wakati akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini uliofanyika leo Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro wakati wa hafla ya Utiaji saini wa Kanuni za Kimkakati za Uwekezaji katika maeneo ya Uhifadhi nchini ambapo amesema Wameanza na TAWA lakini na TFS pia wana maeneo kama hayo ambayo yanahitaji kanuni hozo ili Uwekezaji uweze kufanyika
Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akiwa Kamishna Msaidizi wa Biashara na Huduma za Utalii kutoka TAWA wakifuatilia utiani Saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Watumishi kutoka TAWA mara baada ya hafla ya utiaji saini wa kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi uliofanyika leo Jijini Dodoma
………………………………………………………………………..
Wizara ya Maliasili na Utalii imefungua milango mipya katika Sekta ya Utalii nchini kwa kutia saini ya Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini kwa Wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kutoka ndani na nje ya nchi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro wakati akitia saini kanuni za Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi
nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii amesema utiaji saini huo ni miongoni mwa njia zitakazochangia kuongeza idadi ya Watalii kufika milion 5 na mapato yapatayo bilion 6 ifikapo mwaka 2025 kupitia Sekta ya Utalii nchini.
Kwa mujibu wa Kanuni hizo Wawekezaji wataweza kuwekeza katika maeneo ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu pamoja na Maeneo ya Wazi ya Wanyamapori kwa miaka isiyopungua 25.
Akizungumza kabla ya utiaji saini huo, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kanuni hizo zimelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao hata watalii watakaokuja katika maeneo hayo ni Watalii wenye fedha nyingi ikiwemo watu maarufu duniani.
Amesisitiza kuwa kanuni hizo zitawezesha Wawekezaji hao kujenga mahoteli katika maeneo ya Uhifadhi pamoja na kuweka miundombinu ya Utalii itakayosaidia kuwavutia Watalii wengi kutembelea katika maeneo hayo.
Awali amesema kanuni hizo ni mpya na uwekezaji huo katika maeneo hayo utakuwa wa aina yake kwa vile umelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa watakaowavutia Watalii matajiri hali itakayopelekea pato la taifa kuongezeka maradufu kupitia sekta ya utalii nchini.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali ( Mstaafu) Hamis Semfuko amesema utiaji saini wa kanuni ni moja ya hatua muhimu ya kupanua fursa zitokanazo na sekta ya utalii nchini.
” Tuliamua kuja na wazo hili ili Wawekezaji wenye mitaji mikubwa waweze kuwekeza katika maeneo ya Uhifadhi ambapo awali uwekezaji wa namna hii ulikuwa hauwezekani” alisisitiza Mwenyekiti huyo Meja Jenerali ( Mst) Semfuko
Kwa upande wake , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi amesema atahakikisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ( TFS ) nao wanasaini kanuni za namna hiyo nao waweze kuwavutia Wawekezaji kuwekeza katika maeneo yao kwa vile wa maeneo yenye sifa kawa yalivyo ya TAWA