Mmoja wa wachezaji watoto wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Shufaa Twalib akijiandaa kupiga mpira akiwa kwenye Mazoezi yaliyofanyika Mwisho wa wiki katika viwanja vya klabu ya gofu Lugalo kujiandaa na Mashindano hayo Jijini Dar es Salaam.
***********************
WATOTO ZAIDI YA 40 KUTOKA KLABU ZA GOFU ZA MOROGORO, DAR ES SALAAM GYMKHANA NA WENYEJI LUGALO WANATARAJIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA WATOTO (JUNIOR GOLF TOURNAMENT 2021) ILIYOANDALIWA NA KLABU YA GOFU LUGALO.
SHINDANO HILO LINATARAJIWA KUFANYIKA JUMAPILI YA MEI 16,2021 HUKU LIKIHUSISHA WACHEZAJI WENGINE WA RIDHAA KAMA SEHEMU YA KUWAUNGA MKONO WATOTO AMBAO NDIO CHIMBUKO LA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA.
AKIZUNGUMZIA SHINDANO HILO AFSA HABARI WA KLABU YA GOFU LUGALO KAPTENI SELEMANI SEMUNYU ALISEMA KWASASA KLABU INAWEKA NGUVU KUBWA KATIKA KUENDELEZA VIPAJI VYA WATOTO AMBAVYO KIMSINGI WAMEKUA NA UHABA WA MASHINDANO UKILINGANISHA NA MAKUNDI MENGINE.
‘’HII NI NAFASI NZURI TAREHE 16 JUMAPILI TUTAKUWA NA MASHINDANO NA TUNATARAJIA WATOTO KUTOKA KLABU YA GOFU YA MOROGORO KLABU YA GOFU YA DAR ES SALAAM GYKHANA NA WENYEJI HAPA LUGALO ITAKUWA MWANZO WA KUONA NA KUTAMBUA UWEZO WAO NJE YA KLABU ZAO’. ALISEMA KAPTENI SEMUNYU’
AIDHA MWALIMU WA WATOTO WA LUGALO ATHUMANI CHIHUNDU ALISEMA WAO KAMA WENYEJI WA SHINDALO WAMEJIANDAA VIZURI KUIWAKILISHA KLABU NA HATA KULETA USHINDANI MKUBWA KWENYE GOFU.
‘’UNAJUA MCHEZA KWAO UTUNZWA HAPA NDIO NYUMBANI NA HAKUNA WACHEZAJI WATOTO WENGI TANZANIA HII, NI LUGALO TU HAWA WENGINE WANACHEZA LAKINI HAPA NI CHUO‘’. ALISEMA CHIHUNDU.
AIDHA ALISEMA WANAFUNZI WALIOJIANDIKISHA KUSHIRIKI KATIKA KLABU YAKE HADI SASA NI 32 NA BADO ANAENDLEEA KUSAJILI WENGINE KWANI WAO NI WENYEJI NA WANATAKIWA KUONYESHA MFANO WA WINGI KWA WACHEZAJI KUTOKA KLABU NYINGINE.
‘’KWA HAPA LUGALO WATASHIRIKI 32 NA JUNIOR’S WOTE NILIONAO SAHIVI NI 45 LAKINI WALE WALIOFUDHU KABISA WA KUCHEZA 18 ALL’s WAKO 20, PIA KUNA WENGINE WANACHEZA VIWANJA TISA WAKO 16 NA WALE WANAOCHEZA VIWANJA VITATU WAKO SABA’’
AKIZUNGUMZA NA GAZETI HILI KATIBU WA CHAMA CHA GOFU TANZANIA TGU BONIFACE NYITI ALISEMA WAMEFURAHISHWA NA SHINDANO HILO LA WATOTO NA HIVYO KUTOA WITO KWA VILABU VINGINE KUWEKA NGUVU PIA KATIKA KUNDI HILO KWA UHAI WA MCHEZO.
‘’TUMEFURAHI KUONA SASA KLABU INAENDA VIZURI NA SASA KUWEKA SHINDANO LA WATOTO KWA HIYO SISI KAMA TGU TUMEONA TUSHIRIKISHE NA KLABU NYINGINE ILI KULETA HAMASA’’
KWA NYAKATI TOFAUTI MOJA YA WADHAMINI WA SHINDANO HILO MARYANE MUGO NA KEN MBAYA WAMESEMA WATAENDELEA KUWEKA NGUVU KATIKA KUNDI HILO NA KUAHIDI KUTOA FURSA KWA WACHEZAJI WATOTO HAO KUSHIRIKI MASHINDANO KENYA NA ZIMBABWE KWA UFADHILI WAO.