Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza wakati wa kufungua wa Jukwaa la wakurugenzi jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dodoma kwa kuwatanisha wadau kutoka asasi za kiraia kujadili na kuichambua ripoti ya CAG.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh (kulia) wakisikiliza michngo mbalimbali na maswali kutoka kwa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wadau kutoka CSOS na Kamati za Bunge walishiriki kwenye mkutano huo.
…………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
FOUNDATION for Civil Society (FCS) kwa kushiriana na WAJIBU Institute of Public Accountability kupitia Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia Nchini (AZAKI) limekutana Jijini Dodoma kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Lengo ni kuweza kupata uchambuzi wa Taarifa hiyo na kuweza kuchukua hatua ili kuboresha uwajibikaji,uwazi katika kuboresha utendaji kwa Serikali za Mitaa na Serikali kuu.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya Foundation for Civil society (FCS)Francis Kiwanga wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Jukwaaa hilo ambalo limeshirikisha Wadau mbalimbali wa maendeleo.
Akiongea katika Mkutano huo,alisema kuwa Kama Asasi za kiraia wamekuwa wakifanya kazi na Serikali ili kuwasaidia wananchi katika suala zima la uwazi na uwajibikaji kwa maslahi mapana ya Nchi na kuongeza kuwa nguvu kubwa inahitajika kutoka kwa wananchi katika kufuatili na kuhoji juu ya miradi iliyokamilika na haitumiki.
“Sisi kama wadau wa maendeleo tunahimiza Serikali kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuokoa hasara inayojitokeza ,hii itasaidia kuokoa fedha nyingi mfano Asilimia 36 ya miradi iliyokamilika Nchini haiwezi kutumika licha ya kugharimu rasilimali nyingi za fedha,”alisema na kuongeza;
“Tunashukuru Sana kwa kuwa Serikali imekuwa ikitupa ushirikiano pale tunapohitaji,Pamoja na hayo jamii imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatupa ushirikiano na kutupa urahisi wa kutimiza majukumu yetu Kama asasi za Kiraia,”alifafanua.
Mbali na hayo alieleza Kuwa kwa kuona umuhimu wa maendeleo kwa jamii ,asilimia 15 ya AZAKI zinawajibika Katika ufuatiliaji wa miradi ya maji nchini ili kuwasukuma watendaji kuwa wabunifu Katika kutatua kero kubwa ya Uhaba wa maji nchini.
“Kilio kikubwa kwa Wananchi hususani wanawake ni maji,asilimia 35 ya miradi ya maji nchini imetumia pesa nyingi lakini haijakamilika na ikitokea imekamilika basi haitoi maji, hali hii inapaswa kuangaliwa upya ili kuisaidia Serikali kutopoteza fedha kwa matumizi yasiyo na tija,”alisema.
Licha ya hayo alisema kuwa ili AZAKI hizo ziweze kufanikiwa,ushirikishwaji wa Wananchi Katika maeneo yote unahitajika ili kuongeza muda mwingi nguvu Katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
“Tutachukua maoni ya Wana AZAKI na kuyafanyia kazi,tunatarajia kuona kila miradi ya maendeleo iliyopo kwenye jamii inafanikiwa ,”alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Mstaafu ambaye Taasisi yake imefanya uchambuzi wa Ripoti hiyo , amempongeza CAG Charles Kichere kwa Ripoti nzuri iliyosheheni jumla ya Ripoti 21 ambapo kati yake 15 ni masuala ya uwajibikaji na 9 za Mahesabu.
Amesema, kumekuwepo na suala la kuongezeka kwa hati chafu na kwamba suala hilo linaonyesha kuwepo na shida katika suala la Mahesabu huku akieleza kuwepo kwa udhaifu katika ukaguzi wa ndani.
Aidha amewaomba wananchi kuhakikisha wanaimarisha masuala ya uwazi na uwajibikaji katika kuikosoa Serikali.