Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anaeshughulikia masuala ya Afrika James Duddridge mara baada kuwasili kituo cha Afya Mwera Wilaya ya Kati kuonaa huduma za Vijana zinazotolewa kupitia Mashirika ya misaada ya Ungereza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anaeshughulikia masuala ya Afrika James Duddridge (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakitembelea Kituo cha Afya Mwera kuona huduma zinazotolewa kituoni hapo.
Daktari Mkuu wa Kituo cha Afya Mwera Khadija Soud Hemed akimpa maelezo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anaeshughulikia masuala ya Afrika James Duddridge kuhusu huduma wanazozitoa kwa upande wa IRCH, Uzazi wa Mpango na huduma rafiki kwa Vijana kupitia Mpango wa Afya Jumuishi katika Kituo cha Afya Mwera.
Mshauri nasaha Kituo cha Afya Mwera Bi. Laurie Ali Abdulla akimpatia maelezo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anaeshuhulikia masuala ya Afrika James Duddridge (hayupo pichani) kuhusiana na huduma wanazopatiwa Vijana kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anaeshuhulikia masuala ya Afrika James Duddridge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya kutembelea Kituo cha Afya Mwera kuona jinsi ya misaada inayotolewa na Mashirika ya Uingereza inavyofanya kazi .
Picha na Makame Mshenga.
……………………………………………………………………………
Na Issa Mzee Maelezo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika James Duddridge amesema ataendelea kushirikiana na Wizara ya afya Zanzibar katika kuhakikisha huduma bora za afya zinaendelea kuimarika nchini.
Akizungumza katika ziara yake alipotembelea kituo cha afya Mwera, Wilaya ya kati Unguja, kuona huduma zinazotolewa hasa kwa upande wa afya ya Mama na Mtoto.
Katika ziara hiyo ambayo pia ililenga kuona jinsi gani misaada mbalimbali ya afya inayotolewa na nchi yake imeweza kuwasaidia wananchi wa Zanzibar kupitia washirika mbalimbali ikiwemo mradi wa huduma za afya ya uzazi kwa wanawake, wananume,vijana,walemavu na waathirika wa ukatili wa jinsia pamoja na shirika linaloshughulikia watoto ili kuweka ustawi mzuri wa jamii Zanzibar.
Waziri James alieleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa na wafanyakazi wa kituo cha afya cha mwera hasa elimu ya uzazi wa mpango ambao tayari umeanza kufahamika vizuri na wanajamii pamoja na mikakati ya kusaidia watoto ambayo imesaidia katika kupunguza mimba za utotoni nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika amewapongeza wafanya kazi wa afya pamoja na wadau wengine kwa kufanya kazi nzuri katika kuhakikisha ustawi mzuri wa jamii unapatikana hasa kupitia uzazi wa mpango na uimarishwaji afya ya mama na mtoto.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Waziri wa Afya,Ustawi wa jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema ziara ya Waziri huyo inafaida kubwa katika sekta afya kwani ameahidi kuisaidia Zanzibar katika sekta ya afya ikiwemo taaluma.
Amesema kuwa huduma bora zinazotolewa kituoni hapo zimemhamasisha Waziri James na ameahidi kuendelea kutoa msaada zaidi hasa katika suala la afya ya mama na mototo pamoja na wajawazito ambao wanahitaji huduma na uangalizi zaidi wa kiafya.
“Nchi ya Uingereza imekuwa na msaada mkubwa kupitia washirika wake katika sekta ya afya Zanzibar imetusaidia kuwapatia wafanyakazi ambayo yamewawezesha kutoa huduma bora kwa kina mama wengi na kuokoa maisha yao katika vituo mbalimbali vya afya Zanzibar ” alisema Waziri.
Akizungumzia kuhusu mimba za utotoni amesema kuwa tatizo hilo bado lipo ijapokuwa limepungua kwa asilimia kubwa tofauti na miaka iliyopita kutokana na jitahada mabalimbali za kutoa mafunzo katika maeneo ya Mjini na Vijini.
Aidha amewapongeza viongozi wa dini kwa kusaidia serikali katika jiihada za kutoa elimu kuhusu madhara ya mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya mara kwa mara kwa watoto wakati wakujifungua.
Pia Waziri Mazrui amesema bado serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya Mwera pamoja na vituo vingine Unguja na Pemba.
Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja,Mkuu wa Wilaya Kati Unguja pamoja na wadau mbalimbali wa afya ikiwemo shirika la kushughulikia watoto duniani.