Home Mchanganyiko ANORD MVAMBA MWENYEKITI MPYA UVCCM MKOA WA IRINGA

ANORD MVAMBA MWENYEKITI MPYA UVCCM MKOA WA IRINGA

0


Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba alisema kuwa ataendeleza maono ya mwenyekiti mstaafu ya kuhakikisha vijana wanakuwa na umoja na mshikamano.Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba akipongezwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.

 

Mjumbe wa umoja huoAizack Kikoti akipiga kura katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo


Na Fredy Mgunda,Iringa.

UMOJA wa vijana wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Iringa umepata mwenyekiti mpya baada ya kufanya uchaguzi wa
kuziba nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo
Kenani Kihongosi kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha mkoa Arusha.

Katika uchaguzi uliofanyika
katika ukumbi wa chuo cha chama cha mapinduzi (CCM) Ihemi uliopo wilaya ya Iringa,wajumbe
wa baraza hilo walipigia jumla ya kura 183 na kuthibisha kuwa Anord Mvamba amechaguliwa
kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya ya umoja wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.

Akitangaza
matokeo ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti,msimamizi wa uchaguzi huo mjumbe
wa halmashauri kuu ya taifa MNEC wa njombe Fidelis Lumato alimtangaza Anord  Mvamba kuwa ndio mwenyekiti mpya baada ya
kupata jumla ya kura 181 za kutoka kwa wajumbe wote wa umoja huo.

Alisema kuwa
jumla ya kura 329 zilipigwa na hakuna kura halali zilizoharibika hivyo mshindi
wa kwanza Anord Mvamba alipata 181 na mshindi wa pili Fatma Rembo alipata 123
huku wa tatu Iazack Mgovano alipata kura 25

Alimalizia
kwa kuwaomba vijana wote wa umoja huo kuvunja makundi yote waliyokuwa nayo na
kuanza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuijenga jjumuiya hiyo kuwa
imara kama ilivyokuwa awali.

Baada ya
ushindi huo mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba alisema kuwa ataendeleza
maono ya mwenyekiti mstaafu ya kuhakikisha vijana wanakuwa na umoja na mshikamano.

Aliwataka
vijana kuvunja makundi yote yaliyotokana na uchaguzi ili kuhakikisha wanakijenga
chama na kutafuta fursa mbalimbali zitakazowainua kiuchumi.

Awali akitoa
nasaa zake kwenye mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya
mwenyekiti wa umoja wa vijana wa mkoa wa Iringa, uliofanyika katika chou cha Ihemi
,Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM mkoani humo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha
Kenani Kihongosi alisema kuwa ili kuwa na jumuiya ya vijana bora ambayo itapika
vilivyo viongozi bora ni lazima kuhakikisha wanaendeleza ushirikiano ulikuwepo
kwa viongozi wa chama na serikali.

Alisema kuwa
kiogonzi wa umoja wa vijana akiendekeza Majungu, makundi na mpenda rushwa
hawezi kuwa kiongozi bora kwenye kuimalisha umoja wa vijana ambao ndio tanuli
la kuwapika viongozi bora.

Kihongosi
aliongeza kwa kuwashauri viongozi wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa kuendelea
kuilinda ilani ya chama cha mapinduzi na katiba ya serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ili kudumusha umoja na amani ambao umedumu kwa miaka
mingi.

Aliwaomba
viongozi waliochaguliwa kuingoza jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Iringa Uchaguzi
usiwagawe bali ukawaunganisha upya kuwa na umoja utakaodumu kwa kipindi chote
watakacho kuwa madarakani

Kwa upande
wake kamisaa wa chama cha mapinuzi (CCM) wilaya ya Iringa ambaye pia ni mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii
kujiongezea ufahamu badala ya kufanya mijadala ambayo huleta uchonganishi kwa
taifa na jamii.

Alisema kijana
mwenye maono huondoa uoga na katika kutafuta maendeleo na hutumia mitandao ya
kijamii ili kujijengea uelewa wa kuchanganua masala mabalimbali ya maisha  pamoja na jamii inayomzunguka .