Waziri wa ardhi nyuma na maendeleo ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi akimkabidhi hati ya umiliki ardhi kwa ajili ya uwekezaji, Mkurugenzi mtendaji wa Pan Tanzania Agriculture Development Bi. Dior Feng ambao wanakwenda kuwekeza Mkoani Lindi kwenye zao la Muhogo tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa ardhi nyuma na maendeleo ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati za umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa makampuni 14 yanayokwenda kuwekeza katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Anjelina Mabula akizungumza mara baada ya Waziri Lukuvi kukabidhi hati za umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa makampuni 14 yanayokwenda kuwekeza katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evalist Ndikilo akizungumza mara baada ya Waziri Lukuvi kukabidhi hati za umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa makampuni 14 yanayokwenda kuwekeza katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma, ambapo Mkoa wake ni moja ya Mkoa uliopokea wawekezaji tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji hapa nchini TIC, ambaye ni Mkurugenzi TIC kanda ya kati Bw. Abubakar Ndatwe akizungumza wakati wa Waziri Lukuvi kukabidhi hati za umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa makampuni 14 yanayokwenda kuwekeza katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa ardhi nyuma na maendeleo ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi …..akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Mkoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma pamoja na wawekezaji wanaokwenda kuwekeza katika Mikoa hiyo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji tukio hilo limefanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imekabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa makampuni 14 ya ndani na nje ya nchi yanayotaka kuwekeza katika sekta tofauti hapa nchini katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi na Kigoma mara baada ya kukamilisha taratibu za umiliki wa ardhi katika maeneo wanayotaka kuwekeza.
Akikabidhi hati hizo kwa makampuni hayo kwa niaba ya serikali Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvu ameyahakikishia makampuni hayo kuwa serikali itatoa kila ushirikiano kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kuwekeza hapa nchini.
“Niwahakikishie wawekezaji hii nchi ni salama kwa uwekezaji na tunataka wawekezaji zaidi kuja kuwekeza hapa nchini na sisi hatutakuwa kikwazo kwenu na mtu yeyote anayetaka kuwekeza aje na akikutana na urasimu kwenye ardhi nitumie hata meseji, kwani urasimu wote tumeondoa” amesema Mhe. Lukuvi.
Akitolea mfano wa moja ya kampuni ambayo ni Morogoro Sugar iliyopata ardhi hekta 4000 inayotaka kuwekeza katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari Mkoani Morogoro, amesema kiwanda hicho kitakuwa msaada mkubwa kwani kitazalisha ajira nyingi mashambani na kiwandani huku kikiwanufaisha wakulima wa miwa ambao walikuwa wakikosa soko.
“Sio ajira na kuwanufaisha wananchi ambao kwa muda mrefu walikuwa wakikosa soko la miwa hatimaye kuharibika pia naamini tatizo la sukari linakwenda kuisha kabisa hapa nchini kwani uwekezaji huu ni mkubwa” amesema.
Amesema serikali imejipanga kupokea wawekezaji hapa nchini ambapo ametoa onyo kali kwa watendaji ambao watajaribu kukwamisha wawekezaji kwa kuweka urasimu katika maombi ya ardhi huku akiagiza ombi lolote la muwekezaji lisikae zaidi ya wiki mbili bila kupatiwa majibu.
“Katibu upo hapa na kamishna wa ardhi nataka ndani ya wiki mbili ombi lolote la ardhi kwa muwekezaji liwe limepatiwa majibu, na ile tabia ya kusubiri maombi yawe mengi ndio mpitie kuanzia leo sitaki, kila wiki mkutane kupitia maombi yaliyotumwa hata kama machache” amesema.
Pia ameagiza wakuu wa vitengo vya ardhi katika mikoa au Wilaya yenye wawekezaji waliokabidhiwa hati hizo kuhakikisha kesho wanakwenda kuonyeshwa maeneo yao kwa ajiri ya kuanza shughuli katika maeneo hayo.
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amewataka wawekezaji hao kwenda kuyaendeleza maeneo watakayo kabidhiwa na sio kwenye kuyaacha bila kuyaendeleza au kutumia ardhi hizo kuomba mikopo benk na kwenda kuwekeza sehemu nyingine kwa kutumia ardhi hiyo kama mtaji.
“Haya maeneo yakaendelezwe maana wengine wanaomba kama eneo la uwekezaji lakini anakwenda benk anachukua mkopo anakwenda kujenga apatimenti Dubai hii sio sawa tutakunyang’anya” amesema.
Aidha ametaka kufanyika kwa ukaguzi katika mkoa wa Dar es saalam katika maeneo yote ambayo yalitengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuona kama yanatumika ndani ya vibali vya maombi yao na yatakayokutwa yanatumika kinyume taratibu za kuyachukua maeneo hayo zifanyike.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evalist Ndikilo amesema wamejipanga kuhakikisha wanawapokea wawekezaji katika mkao huo na kubainisha kuwa kwa sasa Pwani imekuwa na mwamko katika uwekezaji ambapo hadi sasa wanaviwanda 1400 huku akibainisha kuwa katika maeneo ya uwekezaji huduma za kijamii zote zinapatikana.
Nao mwakilishi wa kampuni ya Pan Tanzania Agriculture Development bw. Reyson Luka amesema wamejipanga katika uwekezaji kwenye Mkoa wa Lindi ambapo wanakwenda kuwekeza katika kilimo cha mihogo na kiwanda cha kuchakata mihogo pia watatoa elimu kwa wananchi kulima zao hilo kwani soko lake ni kubwa sana nchini China.