Home Mchanganyiko IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU TEDDY MAPUNDA NYUMBANI KABLA YA MAZISHI KATIKA MAKABURI...

IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU TEDDY MAPUNDA NYUMBANI KABLA YA MAZISHI KATIKA MAKABURI YA KWA KONDO BAHARI BEACH DSM

0

Mwili wa marehemu Teddy Mapunda akiwasili nyumbani kwa ajili ya Ibada maalum ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwakwe Kunduchi Kilongawima  leo kabla ya mazishi yaliyofanyika makaburi ya kwa Kondo Bahari Beach jijini Dar es Salaam hukumtoto wa Marehemu Teddy Mapunda akiwa amebeba msalaba.

Viongozi na watu mbalimbali maarufu wamehudhuria katika ibada hiyo ya mazishi.

Waombolezaji ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Motange Limited iliyokuwa ikimilikiwa na Marehemu Teddy Mapunda na Mumewe Nestor mapunda wakiwa wamebeba mashada ya maua wakielekea eneo la kufanyika ibada nyumbani kwake Kunduchi Kilongawima.

Baadhi ya waombolezaji ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Motage Limited wakiwa wamebeba jeneza kuelekea eneo la ibada ya mazishi nyumbani kwake Kunduchi Kilongawima.

Mume wa marehemu Teddy Mapunda Nestor Mapunda kushoto na mwanaye Teddy Mapunda wakiongozana na waombolezaji wengine kuelekea kwenye eneo la kufanyika ibada ya mazishi ya marehemu Teddy Mapunda Nyumbani kwake Kunduschi Kilongawima.

Waombolezaji wakiwa wamebebajeneza.

Waombolezaji wakiwa wamebeba mashada ya maua.

Waombolezaji wakiingia na mwili wa marehemu Teddy Mapunda nyumbani kwake kwa ajili ya ibada ya mazishi.

Mume wa Marehemu Teddy Mapunda akiwa na waombolezaji wengine tayari kwa ajili ya ibada ya kumuombea marehemu Nyumbani kwake Kunduchi Kilongawima jijini Dar es salaam.

Mwili wa Marehemu Teddy Mapunda ukiwekwa eneo maalum kwa ajili ya kuanza ibada ya kumuombea kabla ya mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya kwa Kondo Bahari Beach jijini Dar es salaam leo. 

Waombelezaji mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo.

Baadhi ya mapadre wakijiandaa kwa ajili ya kuendesha ibada ya mazishi ya marehemu Teddy Mapunda iliyofanyika nyumbani Kunduchi Kilongawima jijini dar es salaam.

Picha mbalimbali zikionesha waombolezaji waliohudhuria katika ibada hiyo ya mazishi.