Home Michezo CHELSEA YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA YAICHAPA 2-0 REAL MADRID

CHELSEA YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA YAICHAPA 2-0 REAL MADRID

0
WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Madrid usiku wa Jumatano Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na Timo Werner dakika ya 28 na Mason Mount dakika ya 85 na kwa matokeo hayo, The Blues inatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Madrid.
Sasa Chelsea itakutana na Manchester City katika fainali ya timu za England tupu Mei 29 Uwanja wa Atat├╝rk Olimpiyat Jijini ─░stanbul nchini Uturuki.

Manchester City yenyewe imefika fainali baada ya kuitoa PSG ya Ufaransa kwa jumla ya 4-1, ikishinda 2-1 Paris wiki iliyopita na 2-0 Uwanja wa Etihad jana.