Katibu wa NEC Idara ya Uhusiano wa Kimataifa CCM Kanali Ngemela Lubinga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa Kampeni Kata ya Janda Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.
… …………………………
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa na Uhusiano ya Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga akiwa katika mikutano ya hadhara katika kata ya Janda na Bukuba kumnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Buhigwe – Kigoma Ndg. Felix Kavejuru ameahidi CCM itahakikisha inakamilisha mradi wa kuunganisha umeme katika vijiji vyote vya Jimbo la Buhigwe.
Akifafanua kuhusu ahadi hiyo Ndg. Ngemela Lubinga amesema tayari Vijiji 38 vimeunganishwa na umeme na bado vijiji 6 tu na hivyo Chama kitahakikisha kupitia Serikali yake mradi wa kuunganisha umeme katika Vijiji vilivyobaki ikijumuisha Vijiji vya Janda na Mnyegera unakamilika haraka.
_”Wananchi wa Buhigwe mnabahati sana kuwa na Mwalimu Kavejuru kama Mgombea wa Ubunge hapa, naomba tumpe kura zote za ndio, ili maendeleo yaje hapa Buhigwe kwa kasi”._ amesisitiza Ndg. Lubinga
Aidha, Ndg. Felix Kavejuru Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo hilo la Buhigwe ameendelea kuahidi kuwa atakuwa mnyenyekevu, mfuatiliaji na mtumishi mwema kwa wananchi wa Buhigwe.
Huu ni muendelezo wa Mikutano ya Kampeni katika Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma ambapo kuna Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi ya Ubunge baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Philip Isdori Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMACHA MAPINDUZI