Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Wiki Moja ya Kuwajengea uwezo, maarifa na ustadi katika masuala ya Mikataba. Mafunzo hayo yanafanyika Jijini Dodoma na yameratibiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chama cha Wahandisi Elekezi (ACET). Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo haya ni Mdahisi Marco Benedict Kapinga anayetambuliwa na FIDIC kama Mkufunzi
…………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Maalum
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa amesema, mafunzo wanayopewa Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, siyo tu yatawajengea uwezo na maarifa zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao, bali pia yatawawezesha kuishauri vizuri Serikali.
Dkt. Longopa ameyasema hayo leo May 3,2021 wakati akifungua kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi, mafunzo ya siku wiki moja kuwajengea uwezo, maarifa na utaalamu zaidi Mawakili zaidi ya 20 wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Dkt. Longopa, katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, Mawakili wa Serikali watapatiwa utaalamu na nyezo za matumizi ya Mikataba FIDIC iliyomo katika Kitabu Chekundu (Conditions of Contract for Constraction) na Kitabu cha Njano. ( Conditions for Contract for Plant and Design Build)
Mikataba hii ya Kitabu Chekundu na Kitabu cha Njano hutumika pia kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kama Mradi wa Kufua Umme wa ‘Julius Nyerere Haydro- Power’ na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR).
“Nimatumaini yangu kwamba, mtashiriki kikamilifu katika mafunzo haya ambayo yatawasaidia sana, siyo tu katika kuwaongezea elimu, maarifa na ustadi katika utekelezaji wa majukumu yenu wakati kutoa ushauri, wakati wa majadiliano, wakati mnapo pekua upekuzi wa mikataba au wakati wa usimamizi wa mikataba na uuandaaji wa Sheria bali pia yatawasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yenu ya Kila siku” akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aidha Dkt. Longopa ameeleza kuwa, mafunzo endelevu ya muda mrefu na muda mfupi kwa Mawakili wa Serikali na Kada nyinginezo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ni muhimu na yanahitajika sana kwani licha ya kuwasaidia Mawakili lakini yataisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi kwa mafanikio na pia katika kuhakikisha Thamani Halisi ya Fedha inapatika kupitia miradi ya maendeleo ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Kwa upande wake, Mkufunzi Mkuu wa mafunzo hayo na anayetambuliwa na ‘ Federation of Consulting Engineers’ (FIDIC) Mhandisi Marco Benedict Kapinga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, amesisitiza kwamba, mafunzo hayo yatawawezesha Mawakili wa Serikali pamoja na mambo mengine namna ya kulinda maslahi ya Taifa lakini pia yanawajengea uwezo na wao wakuja kuwa wakufunzi kwa mawakili wengine.
Kama sehemu ya mafunzo Mawakili hao watapata fursa ya kuutembelea mradi wa SGR kama sehemu ya kupata uelewa zaidi.
Mawakili hao wanatoka katika Idara ya Mikataba na Makubaliano, Idara ya Uandishi wa Sheria, Idara ya Uratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria na Kitengo cha Manunuzi.