Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha kamati hiyo kinachoendelea leo kwa njia ya Mtandao.
Katibu wa Kanda Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai akimsikiliza Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin Muturi wakati wa kikao cha Kamati hiyo kinachoendelea leo kwa njia ya Mtandao katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.
Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika wakishiriki kikao cha kamati ya utendaji kinachoendelea leo katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma kwa njia ya Mtandao.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)