Home Mchanganyiko UNDP YATOA KOMPUTA ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40

UNDP YATOA KOMPUTA ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40

0
Mkurugenzi wa Taha Jacqueline Mkindi  akimkabidhi komputa 10 zilizotolewa Kama zawadi na washirika wao ambao ni UNDP kwa meneja wa shule ya  sekondari shepherds Lucy Moses tukio lililofanyika juzi katika viwanja vya shule hiyo iliopo Katika kata ya Mlangarini Wilayani Arumeru
Mkurugenzi wa Taha  Jacqueline Mkindi akiongea na wanafunzi,walimu na baadhi ya wazazi Katika hafla ya kukabidhi komputa 10 zinazotolewa na UNDP kwa shule ya sekondari Shepherds
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya shepherd wakisikiliza kwa makini (Picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
………………………………………………………………….
Na Woinde Shizza,ARUSHA
WALIMU wa shule mbalimbali wametakiwa kuwafundisha wanafunzi wao elimu ya natharia 
na vitendo ili pindi wanapomaliza masomo yao na kwenda mtaani waweze kujiajiri kirahisi 
na sio kutegemea kuajiriwa 
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Taha Jackline Mkindi jana wakati akikabibidhi komputa 
kumi na vifaa vyake venye thamani ya Shilingi milioni 48 vilivyotolewa na washirika wao ambao ni UNDP kwa ajaili ya kuwapatia wanafunzi wa 
shule ya sekondari Shepherds iliopo katika Kijiji cha Manyire kilichopo katika kata ya 
Mlangarine
Alisema kuwa kazi ya TAHA ni kuhamasisha na kutangaza sekta ya horticulture nchini 
,lakini vilevile pia sekta hii inapendwa sana na vijana,na katika kuhamasisha huku sasa hivi 
hatuangalii tu vijana ambao wanatoka vyuoni lakini tunataka wale vijana ambao wanatoka 
kwenye msingi vijana ambao wapo katika levo ya shule za msingi hadi wale waliopo katika 
shule za sekondari pamoja na wale ambao kabla hawajafika vyuoni.
Alisema kuwa wao kama TAHA wameanzisha mikakati mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi 
wa shule mbalimbali hapa nchini ,ambapo katika kuwagusa hawa vijana ili waweze kuelewa 
kabisa na kupenda sekta ya kilimo kuanzia wakiwa wadogo.
‘’chanzo cha komputa hizi kuletwa hapa kama zawadi ni kwamba sisi kama Taha tulikuja 
kutoa elimu ya kilimo cha mboga na matunda kwa wanafunzi hawa wa shule hii ya sekondari 
ya shepherds baada ya kutoa elimu ,tulikuwa tunawafatilia mara kwa mara n ahata mmoja 
wa washirika wetu alipokuwa kututembelea ambaye ni UNDP tuliamua kumleta hapa 
,alivyokuja na kuona namna wanafunzi hawa wanavyofanya kilimo na kukielezea ,namna 
uhamasishaji wa watoto hawa ulivyo ndio akaadi kuwapa komputa hizi wanafunzi hawa ili 
waendelee kujifunza zaidi maswala ya kilimo “alisema Mkindi
Alisema kutokana na mambo ambayo wanayona wanafunzi hawa wanayafanya yamewapa 
motisha zaidi ya kuendelea kutoa elimu kwa shule zingine na vijana wengine kwani 
wanafunzi hawa wameonyesha wanauelewa mkubwa wa masomo ya sanyansi na 
teknolojia jambo ambalo limewashangaza sana pia wana uelewa wa mazao mbalimbali ya 
kilimo .
Aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwafundisha wanafunzi 
hao na kusema kuwa wanawafundisha watoto hao jinsi ya kujiajiri pindi wanapotoka shuleni 
hapo kwani wanakuwa na elimu ya maarifa na vitendo kwa kilimo na jinsi wanavyoendelea 
kupewa elimu zaidi ndio itawasaidia wao kuwa wadau wazuri wa kilimo hapo baadae,kwani 
kilimo ni mti wa mgongo kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu ya Tanzania .
Kwa upande wake mmoja wawanafunzi wa shule hiyo Kennedy Lomboi aliishukuru Taha 
kwa kuwapa elimu ya kilimo ambapo alisema kuwa wanaimani kabisa pindi watakapo maliza 
elimu yao ya sekondari wanapoenda nyumba kusubiri matokeo wataendelea kujiajiri kwa kufanya kilimo.
Aidha aliishukuru UNDP kwakuona umuihimu wao na kutambua kazi wanazifanya za kilimo 
wanapokuwa shuleni hadi wakaamu kuwapatia zawadi ya komputa ambazo alisema kuwa 
zitawasaidia kuendelea kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo kupitia mitandao 
mbalimbali
 Kwa upande wake meneja wa shule ya shepherds sekondari Lucy Moses aliwashukuru Taha 
kwa kumleta mshirika wao ambaye ni UNDPaliyeweza kuwapatia komputa kwa ajili ya 
wanafunzi waliopo hapo shuleni ambapo aliwahaidi kuzitunza na kuzifanyia kazi wa lengo 
lililokusudia huku akaiwasihi walimu wa shule zingine kujitahidi kutembelea taha na kupata 
ujuzi ambao utawasadiia vijana kujifunza mbinu mbalimbali za kujiajiri pindi wanapo maliza 
shule na sio kutegemea ajira za serikalini