Home Mchanganyiko MKUTANO MKUU MAALUM WA KUMCHAGUA MH.SAMIA SULUHU HASSAN KUWA MWENYEKITI WA CCM...

MKUTANO MKUU MAALUM WA KUMCHAGUA MH.SAMIA SULUHU HASSAN KUWA MWENYEKITI WA CCM WAANZA JIJINI DODOMA

0

Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan  anayetarajiwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM leo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion akiwa kwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula kulia na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwini wakiimba  wimbo maalum wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano huo jijini Dodoma leo Aprili 30,2021

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kushoto na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula wakishiriki kuimba wimbo maalum wa CCM wakati Mwenyekiti Mtarajiwa Mh. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.

Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan  anayetarajiwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM leo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion akiwa kwa pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.

Wenyeviti Wastaafu wa CCM kulia ni Jakaya Kikwete na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Wajumbe wa Kamati Kuu Taifa Dk. Philip Isdori Mpango kushoto na Dk. Hussein Ali Mwinyi wakifuatilia mkutano huo kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mzee Amani Abeid Karume.

Picha mbalimbali zikionesha kundi la muziki la TOT likitumbuiza wajumbe wa mkutano huo maalum unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion jijini Dodoma. 

Mwanamuziki Zuena Mohamed Shilole akiwa katika mkutano huo pamoja na wasanii wenzake.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh.Nape Nnauye akiwa katika mkutano huo.