Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Timu ya Simba imezidi kuusongelea ubingwa wa msimu wa 2021/22 baada ya kuichapa mabao 3-1 Dodoma Jijini Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba walipata bao yao kupitia kwa Chris Mugalu dk.8 na 66 huku Luiz Miquissone dk 55 na bao la kufutia machozi la Dodoma Jiji limefungwa na Kiungo Cleophace Mkandala dk 28.
Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 61 na kuendelea kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania bara na kuwaacha Yanga nafasi ya pili wakiwa na Pointi 57 na Azam FC nafasi ya tatu kwa Pointi 54.