………………………………………………………………………………
Kikosi cha KMC FC kimendelea kujiimarisha leo kulekea katika mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho ( Azam Sports Federation CUP) dhidi ya Dodoma Jiji utakaofanyika siku ya Mei Mosi katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
KMC inaendelea na mzunguko wa 16 wa michuano hiyo ikiwa ni baada ya kupata ushindi dhidi Timu ya Kurugenzi kutoka Mkoani Simiyu kwa kuifunga magoli matano kwa mawili na hivyo kuitoa katika michuano kombe hiyo.
Katika mchezo huo dhidi ya Dodoma Jiji , KMC FC inajipanga vyema kuhakikisha kwamba inakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo na hivyo kupata nafasi ya kuendelee kusonga mbele katika michuano hiyo na hivyo kuchukua kombe hilo.
“ Tunajiandaa kwenda kwenye mchezo mgumu ambao kimsingi ukifungwa ndio unakuwa umeaga michuano hiyo, hivyo kwakulitambua hilo, tunajidhatiti ili kupata matokeo mazuri ambayo yatatupa fursa ya kuendelea mbele kwasababu KMC FC tunalihitaji kombe hilo kwa umuhimu mkubwa sana.
KMC imekuwa na matokeo mazuri katika michezo ya Ligii Kuu soka Tanzania bara hususani katika michezo ambayo imecheza hivi karibuni hivyo kwa uwezo, ubora wa wachezaji na kiwangosafi ambacho wamekionesha katika michezo hiyo, inakwenda kuendeleza katika michuano hiyo ilikuleta chachu ya mafanikio ndani ya Manispaa ya Kinondoni.