NA MAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta amekipongeza chuo cha Uhasibu Arusha{IAA} kwa kuazimisha siku ya muungano kwa kufanya mbio mbio fupi maarufu kama Fun run kuelekea Marathon ya kitaifa inayotarajiwa kufanywa na chuo hicho June mwaka huu na kusema kuwa mazoezi ni afya na yanajenga ushirikiano jambo amablo amevitaka vyo vingine vilivyopo katika mkoa huo kuiga.
Kimanta ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki wa mbio hizo aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa mbio hizo za kilometa 6 ambapo alisema kuwa kwa kuwa na mwendelezo wa mbio hizo watajenga Afya pamoja na kuwa na ushirikiano mzuri utakaopelekea kuijenga Arusha na pia ikiwa ni mwendelezo wa maagizo ya Mhe Rais Samia Suluhu aliyoyatoa wakati akiwa makamu wa Rais.
Alifafanua kuwa um,efika wakati wa kuimarisha vikundi vya mazoezi kwani ni sehemu ya dawa hasa wakati huu ambapo dunia inapita katika changamoto ya Covid 19 na kumtaka mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi kutafuta siku maalum ya vyuo vya Arusha kufanya mazoezi ya pamoja ili kuboresha afya lakini pia kujenga mkoa wao.
“Pamoja na kutafuta siku maalum kwaajili ya vyou kufanya mazoezi lakini pia vyuo vingine viige mfano wa IAA kwani pamoja na kutoa elimu lakini pia wanaboresha afya za wanafunzi wao, watumishi na watu wengine majirani wakiwemo wakuu wa tasisi kwa kufanya mbio hizi,” Alisema Kimanta.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi alikitaka chuo hicho kuendelea kufanya mambo ambayo yataweka wanaarusha pamoja na kujenga afya zao na kuepuka magonjwa nyemelezi na kuwataka wengine waige suala hilo ili kuboresha afya za wanajamii.
Naye mkuu wa chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka alisema kuwa mbio hizo ni mwendelezo wa fun run wanazozifznya kila mwezi kwaajili ya maandalizi yam bio kubwa zitakazofanyika June na kushirikisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ambapo IAA marathon lengo lake kubwa ni kukitangaza chuo kwani ndio msingi mkubwa wa biashara ambapo wanapokuwa wamekikuza chuo watakuwa na mvuto zaidi kwa wateja na hiyo ni moja kati ya mikakati yao kwa kuja na shughuli za kitaifa ambazo zitaweza kuvutia watu.
Alisema pia kwa kupitia mbio hizo wataweza kunyanyua na kukuza vipaji vya kukimbia kwani Tanzania hivi karibuni imekuwa kama kivutio cha watu kufahamiana, kuwa na undugu lakini pia kushereheka zaidi kwani Arusha iko nyanja za juu na maeneo yake ni mazurikwa kufanyia mazoezi ya mbio ndefu kwahiyo wanategemea kwamba italeta upizani mkubwa na wamejipanga kuhakikisha kuwa wale wote watakao waalika watawashindanisha na kutoa mabingwa ambao wataweka rekodi za kitaifa kwenye kilometa 21 na 47,” Alisema Professa Sedoyeka.
Aidha alisema kuwa mazoezi ni muhimu kwani ili mtu aweze kuwa na akili nzuri awe ni mwanafunzi au mwalimu aweze kufundishwa au kujifudha mwili unanafasi kubwa kwani kwa kufanya mazoezi mtu anaweza kuondoa mawazo(stress).
“Pamoja na kuondoa stress lakini pia unajenga mwili kwa kuweka vizuri usawa wa sukari, chumvi na madini mengine yaliypo mwilini pamoja na kuchochea unywaji wa maji ambo unapelekea kuweka misuli, na damu sawa pamoja na kwenda kuondoa yale magonjwa yasiyoambukizika kama sukari, moyo, msogo wa mawazo na mengine,” Alisema
Hata hivyo makamu wa raisi wa chama cha riadha nchini John Bayoa ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki wa mbio hizo alisema kuwa mbio hizo zitakuja kuwa kubwa ikiwa ni pamoja na kuwataka kuwashirikisha wataalamu katika maandalizi ili kuepuka kuja kushinda kukidhi vigezo ambayo itawapelekea kufungiwa .