Naibu Waziri wa Ujenzi Mh Mwita akizungumza na watendaji katika kikao cha taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akizungumzia utendaji kazi na majukumu ya TANROADS kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara katika kikao kazi cha Wakuu wa Taasisi na Wakuu wa idara zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Aprili 24, 2021 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
………………………………………
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara amefanya kikao kazi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ikiwemo TANROADS kwa lengo la kufahamiana na kuangalia utendaji kazi na utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hizo.
Kikao hicho kilichofanyika Aprili 24, 2021 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere , Jijini Dar es Salaam kilihudhuriwa pia na wakuu wa idara mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
Mhe. Naibu Waziri alitoa pongezi kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Partick Mfugale kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miundombinu ya barabara na madaraja na ambayo ilipelekea kupatiwa heshima ya “flyover” maeneo ya TAZARA ambayo inajulikana kama Mfugale Flyover.
Aidha, Naibu Waziri Waitara amesema kwa upande wa magari yanayoharibu barabara pamoja na kuwepo kwa tozo, bado uharibifu unaotokana na uzito wa magari hayo umekuwa mkubwa kwa barabara.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amesema TANROADS itaendelea na jukumu la kutunza barabara na kujenga viwanja vya ndege nchini.