*************************
NA BARNABAS GWAKISA 0621 312 341 (Mr Darajani)
Ninachokiona kwenye hili la michuano mipya ya European Super League, naona hii kitu inapewa nguvu na Marekani.
Ukichunguza wadhamini wa kwanza kuwekeza pesa kwenye mpango huo ni benki kutoka Marekani, JP Morgan Chase & Co.
Kwa mtazamo wangu naona hili fukuto limekua likikua kutokana na pendekezo la muda mrefu nchi ya Marekani kutamani baadhi ya michezo ya Klabu bingwa Ulaya ikachezewe nchini humo, mpango ambao UEFA wamekuwa wakishindwa kuutimiza kwa kuwa nchi ya Marekani haipo bara la Ulaya.
Sasa kwa kuwa Marekani wamekuwa na sauti kubwa sana wameamua kuanzisha chokochoko za chini kwa chini ili hili jambo litimie, ligi mpya ianzishwe ikiwa nje ya shirikisho la soka Ulaya ili wao wapate nafasi ya kuona michezo ya klabu vigogo duniani ikichezwa pia nchini kwao Marekani.
Ukichunguza tena viongozi wa michuano hiyo mipya wengi ni raia wa Marekani, Joel Glazer (Man utd), John Henry (Liverpool) na Stan Kroenke (Arsenal), unategemea watapinga Marekani ikitaka michuano iende kwao?
Ngoja tusubiri tuone nini kitatokea baadae!
Lakini kila nikiwaza UEFA Champions League bila timu vigogo na Ligi kuu Uingereza bila Chelsea, Man city, Tottenham, Liverpool, Arsenal na wale wengine akina Man utd, sijui itakuwaje!
#d1905_uchambuzi