Dkt. Ernest Mbega, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela akisoma risala kwa niaba ya Naibu Makumu Mkuu Chuo Mipango, Fedha na Utawala wa Taasisi hiyo Prof. Charles Lugomela wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya masuala ya kijinsia iliyofanyika Leo 15, Aprili 2021 Jijini Arusha.
Mratibu Msaidizi wa Polisi kutoka katika Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bibi. Happiness Temu akiwasilisha mada kuhusu Hatua na Taratibu za Kufuata mtu anapo kumbana na uzalilishaji wa kijinsia, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya masuala ya kijinsia iliyofanyika Leo 15, Aprili 2021 Jijini Arusha.
Mkurungezi wa Taasisi ya Sasa (Sasa Foundation) Bibi . Yovita Mlay akiwasilisha mada kuhusu hatua mbalimbali za kufuata katika kuvunja ukimya mtu anapokutana na changamoto za ubaguzi wa kijinsia , wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya masuala ya kijinsia iliyofanyika Leo 15, Aprili 2021 Jijini Arusha.
Meneja wa Kituo cha Umahiri katika Ufundishaji na Utafiti Katika Nyanja za Kilimo na Usalama wa Chakula na Lishe (CREATES-FNS) Bibi . Rose Mosha akiwasilisha mada kuhusu Uzalilishaji wa Kijinsia , wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya masuala ya kijinsia iliyofanyika Leo 15, Aprili 2021 Jijini Arusha.
Washiriki wakisiliza watoa mada mbalimbali katika Warsha ya Masuala ya Kijinsia iliyoandaliwa na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na Kituo cha Umahiri katika Ufundishaji na Utafiti Katika Nyanja za Kilimo na Usalama wa Chakula na Lishe (CREATES-FNS) Leo 15 Aprili, 2021 Jijini Arusha.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango ,Fedha na Utawala waTaasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela Prof. Charles Lugomela (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya masuala ya kijinsia iliyofanyika Leo 15, Aprili 2021 Jijini Arusha.
Picha na Orester Julius – CREATES Arusha
………………………………………………………………………………
Na Orester Julius-CREATES-FNS
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango Fedha na Utawala wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela Prof. Charles Lugomela ameipongeza Kamati ya Masuala ya Jinsia ya Taasisi hiyo kwa kuandaa warsha ya kuwajengea uelewa wa pamoja wafanyakazi na wanafunzi kuhusu masuala ya uzalilishaji, ubaguzi wa kijinsia na rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi na masomo.
Prof Lugomela ameyasema hayo leo Aprili 15, 2021 Jijini Arusha wakati akifungua warsha hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na kamati inayoshughulikia masuala ya jinsia ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na Kituo cha umahiri katika Ufundishaji na Utafiti katika Nyanja za Kilimo na Usalama wa Chakula na Lishe (CREATES -FNS).
Naibu Makamu huyo ameongeza kuwa warsha hiyo ni hatua mojawapo ya kupata uelewa kuhusu taratibu, sheria na kanuni za kufuata pale mtu anapokutana na changamoto ya masula ya kijinsia katika eneo la kazi au masomo.
“Warsha hii itawasaidia wafanyakazi na wanafunzi kutambua sheria za nchi na sheria za taasisi zinazoshughulikia masuala ya kijinsia ili kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo ya kazi na masomo” alisema Prof. Lugomela.
Naye Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Bibi. Happiness Temu ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela kwa kuweza kuandaa warsha hiyo muhimu ambayo itasaidia katika kuvunja ukimya na kupunguza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.
Aidha, Mkurugenzi wa Sasa Foundation na Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Bibi Yevita Mlay ameeleza kuwa sasa ni wakati muafaka wa kupaza sauti kwa jamii na maeneo ya kazi kuhusu masuala ya kijinsia ili kuleta chachu ya mabadiliko na kufikia maendeleo endelevu.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Masuala ya Kijinsi ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela Dkt. Josephine Mkunda ameahidi kuendeleza utaratibu wa kuwa na warsha za mara kwa mara ili kuzidi kuwajengea uelewa wafanyakazi na wanafunzi kukabiliana na changamoto za masuala ya kijinsia katika maeneo ya kazi na masomo.
Mwisho