Meneja mkuu wa kiwanda cha kutengeneza Magari mapya cha Kwanza nchini Tanzania GF- Vehicle Assembly Ltd , Ezra ,,,,, akizungumza na wateja wa kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwan wakati wa sherehe ya kutimiza Magari 100 yaliotengenezwa na kiwanda hicho kwa kipindi Cha miezi nne.
Baadhi ya magari yaliyounganishwa katika kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
…………………………………………….
Kiwanda kipcha cha kutengeneza na kuunganisha Magari nchini Tanzania GF vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani leo kimetimiza utengenezaji wa Gai ya miamoja kuanzia kipindi cha mwezi Januari hadi wa nne.
Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 100 kukanyaga aridhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kwa kutembea ,Meneja mkuu wa kiwanda cha hicho ,Ezra Mereng alisema ni kazi ngumu kukamilisha zoezi la uunganishaji na utengenezaji wa magari hayo kwa kuwa Tanzania sisi ndio Kiwanda cha kwanza kutengeneza (kuunganisha) magari
Changamoto ni nyingi kutokana na kutokuwa na wataalamu wengi katika sekta hii ya Magari lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa nje tuliweza kuunganisha magari 10 ya awali na baadae wao wakaondoka na tukabaki na watanzani wenzetu ambao kwa uwezo wa Mungu leo tumefanikiwa kumaliza gari ya 100.
Pia alizitaka Tasisisi za serikali na kagiza magari ambayo hayajaunganishwa na kazi ya kuunganisha ifanyike na viwanda vya ndani ili kukuza pato la taifa na kuweza kuongeza ajira kwa watanzania pia kama nchi itajipatia fedha za kikgeni kwa kuuza nchi jirani Magari yanayotoka Tanzania.
Nae afisa masoko na manunuzai wa kampuni ya uuzaji wa magari ya FG Trucks & Equipments Ltd , Hamis Hasasn ambao ni moja ya wateja walipeleka kazi ya kuunganishiwa Magari yao katika kiwanda hicho alisema Mwanzo wateja walikua hawaamini kama magari hayo yatakuwa na ubora sawa lakini kwa kipindi hiki magari yapo mitaani na yanafanya vizuri alimaliza Hamis
Kiwanda hicho kimeajiri Wafanyakazi 100 ambao ni pamoja wenye ajira za kudumi mikataba pamoja na za muda mfupi