Home Mchanganyiko RAIS MHE.SAMIA SULUHU AAGIZA KUFUNGULIWA KWA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOFUNGWA

RAIS MHE.SAMIA SULUHU AAGIZA KUFUNGULIWA KWA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOFUNGWA

0

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu ameagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungwa na kuwekwa kwa utaratibu wa kufungiwa kwa vyombo vya habari ambavyo havifuati utaratibu.

Ameyasema hayo leo alipowaapisha Makatibu wakuu na Wakurugenzi Serikali Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Samia ameagiza adhabu ziwe wazi kwamba chombo kikifanya kosa fulani adhabu yake ni fulani hali itakayosaidia isionekane kuwa serikali inaminya uhuru wa vyombo vya habari.

“Nasikia kuna vyombo vya habari mlivifungia,vifungulieni lakini wafuate kanuni na miongozo ya serikali na kanuni ziwe wazi”. Amesema Rais Mhe.Samia.