Home Mchanganyiko SERIKALI KUUNDA KAMATI YA WATAALAMU KUHUSU COVID 19

SERIKALI KUUNDA KAMATI YA WATAALAMU KUHUSU COVID 19

0

************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema wataunda Kamati ya wataalamu kuhusu Covid19 na kusema kitaalamu yanayopendekezwa na ulimwengu kuja hapa nchini yapoje.

Ameyasema hayo leo baada ya kuwaapisha Makatibu wakuu na wakurugenzi ndani ya Serikali leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Rais Mhe.Samia Suluhu amesema hatuwezi kujitenga tu kama kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kufanya utafiti wa hapa kwetu.

“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 ulimwenguni”. Amesema Rais Mhe.Samia Suluhu.