Home Mchanganyiko WAANDISHI WANA WAJIBU WA KUITUNZA NA KUIENZI SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

WAANDISHI WANA WAJIBU WA KUITUNZA NA KUIENZI SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

0

Mkurugenzi TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja yaliolenga kuwajengea uwezo wanahabari hao kutambua umuhimu wa Serikali ya umoja wa kitaifa namaridhiano.

Picha ya pamoja ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti Zanzibar walioshiriki katika mafunzo ya siku moja katika ukumbu wa TAMWA Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

***********************************

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa Ally amesema waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kuitunza na kuienzi Serikali ya umoja wa kitaifa ilioasisiwa visiwani  hapa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano kwa wazanzibar wote.

Ameyasema hayo katika ofisi za Chama hicho zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja yenye lengo la kuenzi umuhimu wa maridhiano Nchini.

Alisema uwepo wa maridhiano katika Nchi ni jambo  muhimu ambalo hupelekea  pia Nchi kupiga hatua zaidi kimaendeleo kwa kuwa amani ndio tunu muhimu kwa kila Nchi inayohitaji kukua kiuchumi.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema waandishi wa habari wana wajibu wa kuhakikisha kila mwananchi wa Zanzibar ananufaika na uwepo wa Serikali ya umoja wa kitaifa kwa namna moja au nyengine.

‘’Serikali ya umoja wa kitaifa ni ya watu wote wanahabari kafanyeni kazi muhakikishe kila mtu ananufaika na uwepo wa Serikali hii bila kujali chama chake wala kabila lake’’aliongezea.

Sambamba na hayo aliwakumbusha wanahabari hao kuhakikisha wanaweka usawa kwenye habari zao bila ya kumuumiza yoyote kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya taaluma hio.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka shirika la Internews Alhaj Mwadini alisema wanahabari ni watu muhimu wanaopaswa kufanya kazi zao kuisaidia jamii na Serikali kwa ujumla.

Alisema iwapo wanahabari watatekeleza wajibu wao ipasavyo ni nguzo muhimu ambayo italeta ufanisi na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na hata jamii kiujumla.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja wamesema yamekuja wakati muafaka kwa kuwa Zanzibar ipo kwenye Serikali ya umoja wa kitaifa inayohitaji kutunzwa na kuenziwa.

Miongoni mwao ni Ally Rashid amesema mafunzo hayo yamemsaidia kutambua umuhimu wa maridhiano kwa wanajamii na madhara yake.