Home Mchanganyiko Serikali ipo inafanya kazi vizuri na itaendelea kuwepo, muhimu kudumisha amani –...

Serikali ipo inafanya kazi vizuri na itaendelea kuwepo, muhimu kudumisha amani – RC Wangabo

0

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa salamu zake za Pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi ‘Bakuli’ la Sadaka kwa Padri Canute Mwageni Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme Mjini Sumbawanga muda mfupi baada ya kuchangisha fedha hizo kwaajili ya kuwapatia watoto yatima wa kituo cha Mtakatifu Maria Goreth kilichopo Katandala. Mjini Sumbawanga.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo pamoja na Waumini wengine waliposhiriki Ibada ya Pasaka katika Knaisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Mjini Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwa na Mkewe Bi. Veronica Wangabo wakipokea mchango kutoka kwa waumini waliohudhuria katika ibada ya pasaka iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwa na Mkewe Bi. Veronica Wangabo wakipokea mchango kutoka kwa waumini waliohudhuria katika ibada ya pasaka iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme mjini Sumbawanga.

**********************************

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatoa wasiwasi wananchi Mkoani Rukwa ambao bado wamekuwa wakijiuliza maswali juu ya uelekeo wa serikali na nchi baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17.3.2021.

Mh. Wangabo amesema kuwa tangu nchi hii ipate uhuru mwaka 1961 ni mika 60 imepita na sasa imepata rais wa Sita Mwanamke, tukio ambalo ni la kihistoria na kuongeza kuwa kinamama kwa miaka mingi wamekuwa shupavu katika kuongoza familia hasa malezi ya Watoto na hivyo kuwaomba wananchi wote kuziongoza familia zao kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ilia pate nguvu na Afya na kuleta maendeleo katika nchi yetu.

“Najua kila mmoja wetu sasa hivi anatafakari kwa kina kwamba nchi sasa hivi tunaelekea wapi, niwahakikishie kwamba serikali ipo, inafanya kazi vizuri na itaendelea kuwepo na sisi tupo, tunachotaka sisi ni amani ili nchi iweze kusonga mbele, lakini kikubwa Zaidi niwaombe tuendelee kumuombea Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia, tumuombee san ana tuwaombee viongozi wote wa serikali ili serikali yetu isiyumbe iwe thabiti na kwa maongozi ya Mwenyezi mungu tutafika.”

“Sina shaka, Rais wetu anatutosha, lakini anahitaji kuungwa mkono, mshikamano na amani na utulivu kutoka kwetu, bila ya shaka wanarukwa wote, tunalifanya hili na tumeanza kulifanya na tutaendelea kulifanya la kuleta amani, na tumeshuhudia tuna amani ya kutosha, tuendelee nayo, lakini tusione mtu ana ngeu ama amevunjika mguu kesho ama keshokutwa, mtaleta dosari,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu zake za Pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Mjini Sumbawanga baada ya Ibada ya Pasaka ambapo wakristo wote nchini wanaungana na wenzao duniani kusheherekea sikukuu hiyo.

Aidha, katika kuhakikisha Watoto yatima hawaachwi nyuma Mh. Wangabo alipitisha ‘Bakuli’ kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo ili kupata fedha za kununua baadhi ya mahitaji kwaajili ya Watoto yatima wa kituo cha Mtakatifu Maria Goreth kilichopo Katandala mjini Sumbawanga, ambapo katika mchango huo ilipatikana Shilingi 188,600/= na kuzikabidhi kwa Padri Canute Mwageni Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme Mjini Sumbawanga