
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati askofu Dkt Solomon Massangwa akihubiri katika ibada ya maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka.

Mwinjilist Baraka Mollel wa Usharika wa Ilkiranyi
*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati askofu Dkt Solomon Massangwa amesema ushindi wa Yesu kristo utaleta ushindi wa mtu mmoja mmoja ambao katika kushinda huo mwisho kanisa litashinda, Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Askofu Dkt Massangwa aliyasema hayo katika ibada ya kusherehekea sikuku ya pasaka iliyofanyika kanisa kuu usharika wa Arusha mjini ambapo aliwataka watanzania kuifanya agenda ya umoja wa mataifa ya mwaka 2063 kuwa agenda yao katika familia na kazi zao kwani Tanzania inajengwa na mtu mmoja mmoja.
“Yesu amefufuka kama alivyosema kwa maana hiyo tumeona hakuna cha kumshinda Mungu hivyo katika kufufuka kwake nawasihi muangalie ni wapi mipango yenu iliharibika kwani leo ni siku ya kumuomba Mungu afufue palipo haribika na aifufue Afrika,” Alisema Askofu Dkt Massangwa.
Alieleza Mungu aliyemfufua Yesu yupo tayari yupo tayari kufufua kazi, mahisiano yaliyoharibika, taifa na mengineyo kwa kuyapa maisha mapya na wale waliofikiri haiwezekani tena wataabika kama makuhani walivyoahibika kwa kufikiri wamemmaliza Yesu.
“Nenda na biashara yako kwa Mungu, kazi, ndoa, familia na yeye atakushindia kama alivyomshindia Yesu ambapo walipomuua walifurahi sana kwani walimuona ni mtu hatari lakini siku ya tatu kazi yao ikawa bure, mpango wao ukashindwa,”Alieleza Askofu Dkt Massangwa.
Alifafanua kuwa wanaposema haleluya maana yake wanamsifu Bwana ambaye ameshinda kifo na mpango wa mwanadamu wa kumshinda Mungu.
Kwa upande wake Mwinjilist Baraka Mollel wa Usharika wa Ilkiranyi akihubiri alisema kuwa Pasaka sio ibada ya kihistoria bali ni ibada ya imani ya kutoka katika dhambi na kuingia katika utakatifu.
Alisema kuwa wanasherekea kufufuka kwa Bwana mwokozi wao Yesu kristoa na wanasherehekea sio tu kwa kula vyakula vizuri, kupiga vigelegele na makofi lakini bali ni tendo la kiroho linaloonyesha utu mpya wa mtu kubadilishwa na Mungu baada ya kichukua dhambi zake, madhaifu na taabu.
Mwinjilist Baraka alieleza Yesu ni zaidi ya yule malaika aliyekuwa amelikalia jiwe baada ya kufufuka kwa Yesu, ameyaondoa mawe kwenye maisha yao, dhambi, magonjwa na mateso yote.
“Sio kwetu wakristo tuu kwani Yesu yupo kwaajili ya ulimwengu wote na katika nchi wanasisa wakimpa Yesu maisha taifa litabadika kwani hakuja kwaajili yetu pekee bali kwa wote watakao mwamini, Alieleza Mwijilist Baraka.
Aidha aliwataka wakristo kutokupokea sherehe ya Pasaka kimwili bali wapokee kiroho kama tendo la imani kwani tendo la kiroho halina Historia na wakiamini kiwa Yesu amefufuka kweli maisha yao yatabadishwa na kuondokana na changamoto zinazowakabili hivi sasa.
“Yesu anafanya kila kitu akifufika ndani yetu ataokoa maisha yetu, uchumi wetu, biashara pamoja afya kikubwa ni kumpa nafasi katika mioyo yetu na kumuamini,” Alisema.
Hata hivyo Pasaka ni sherehe yavkiyahudi inayokumbusha jinsi alivyowakomboa waisraeli kutoka katika utumwa wa Kimisri mwaka 1513 kabla ya Kristo ambalo Mungu aliwaagiza waisraeli kukumbuka tukio hilo muhimu kila mwaka katika siku ya 14 ya mwezi wa kiyahudi na wakristo wanaungana wayahudi kusherehekea pasaka ka tendo la kutoka utumwani kwenda nchi ya ahadi.