Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 Bw. Charles E Kichere Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo March 28,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 kutoka kwa Mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia General John Mbung’o leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kupokea ripoti za Mkaguzi Mkuu wa
Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini
Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
pamoja na waliohudhuria hafla ya kupokea ripoti za Mkaguzi Mkuu wa
Serikali na TAKUKURU wakisimama kwa dakika tatu kumkumbuka aliyekuwa
Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya
Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga mara baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Akson baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Rais)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Bw. Charles E Kichere mara baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Bw. Charles E Kichere mara baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Adeladus Kilangi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Bashiri A. Kakurwa mara baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe
Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo
Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe
Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance
Salvatory Mabeyo na viongozi wengine baada ya hafla ya kupokea ripoti
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino
jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe
Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi
28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi
Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job
Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally pamoja na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya hafla ya kupokea ripoti za
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini
Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiongea na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro baada ya
hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na
TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo
Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiaga ili kuondoka eneo la tukio baada ya hafla ya kupokea ripoti za
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika
Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akiongea na viongozi mbalimbali waliohudhuria
hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na
TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo
Jumapili Machi 28, 2021.
PICHA NA IKULU
************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuandaa mfumo madhubuti wa kupambana na Rushwa kwani vitendo hivyo bado vinaendelea katika maeneo mbalimbali.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Ikulu Jijini Dodoma.
“Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo vimezidi kuendelea hivyo ni lazima kuwe na mikakati na mifumo mipya ya kukabiliana navyo”. Amesema Rais Mhe.Samia Suluhu.
Aidha Mhe.Samia amesema atasimama imara katika mapambano dhidi ya Rushwa hasa Rushwa ya ngono ambayo imekidhiri katika maeneo mengi.
Pamoja na hayo amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dr. Charles Kichere kutokuwa na kigugumizi chochote kwenye Shirika analoona halifanyi vizuri kimapato.
“Tukinyamaziana kwa kutazamana sura hatutarekebisha na tutawaumiza Wananchi, naomba sana ripoti yako CAG iwe wazi zaidi, utakaponiletea ukaguzi wa Mashirika naomba uwe wazi zaidi ili tujue tunachukua hatua gani”.Ameeleza Rais Mhe.Samia Suluhu.