Home Mchanganyiko RAIS MH.SAMIA AMPIGA (STOP) MKURUGENZI WA TPA KUPISHA UCHUNGUZI TUHUMA ZA UBADHIRIFU

RAIS MH.SAMIA AMPIGA (STOP) MKURUGENZI WA TPA KUPISHA UCHUNGUZI TUHUMA ZA UBADHIRIFU

0

NA EMMANUEL MBATILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Deusdedit Kakoko kupisha uchunguzi.

Rais Samia amemsimisha Mkurugenzi huyo IKULU Dodoma leo akipokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali Dr. Charles Kichere.

“Kuna ubadhirifu mkubwa Bandarini naomba TAKUKURU ikafanye kazi, nimeletewa ripoti ya ubadhirifu wa Bilioni 3.6″. Amesema Rais Mhe.Samia Suluhu.

Akitoa ripoti mbele ya Rais Samia Suluhu CAG Charles Kichere amesema kuwa katika

“Katika ukaguzi wetu wa mwaka 2019/2020 tumegundua Shirika letu la Ndege limetengeneza hasara mwaka huu ya Tsh.Bilioni 60 ila kwa miaka mitano pia limekuwa likitengeneza hasara.

kuna changamoto ambazo Sarikali inabidi iziangalie ili Shirika letu litekeleze majukumu yake vizuri”.CAG Charles Kichere.

Aidha Rais Mhe.Samia amesema kuwa TAMISEMI kuna upotevu wa fedha, hivyo amemtaka Waziri wa Wizara hiyo alifanyie kazi.

“Waziri uko hapa Jaffo tunaomba uhangaike mara ya mwisho ukishindwa sema tukusaidie, Tamisemi mnachukua fedha nyingi serikali kuu lakini wao hawarudishi”. Amesema Mhe.Samia Suluhu.