***********************************
NJOMBE
Wakazi wa mkoa wa Njombe kwa kushirikiana viongozi wa madhehebu ya dini wameshiriki kwa njia ya sara katika mazishi ya hayati Dkt Magufuli yanayofanyika wilayani Chato mkoani Geita kwa kufanya ibada maalumu ya kumuombea rais aliyefariki dunia akiwa madarakani pamoja na rais wa sasa Samia Suluhu Hasan kwa lengo la kuikabidhi nchi kwa mungu katika kipindi hiki kigumu na nyakati nyingine.
Akitolewa dua shekh mkuu wa wilaya ya Njombe Shaban Dingadinga,Mchungaji wa kanisa kuu la KKKT mkoa wa Njombe Nelson Godiwe pamoja mchungaji wa kanisa la TAG mkoani humo Zephania Tweve wanasema watanzania wanapswa kuondoa hofu kwa kitendo cha kuondokewa na kipenzi chao kwani mungu ameshamuandaa Samia Suluhu Hassan kuja kuendeleza kazi iliyokuwa ikifanywa na rais Magufuli enzi za uhai wake.
Viongozi hao wa dini wanasema kilichotokea Tanzania kilitokea Israel baada ya Mungu kumchukua nabii musa wakati wana wa Israel wakiwa bado wanamuhitaji na kisha kumleta Joshua ambaye alikuwa msaidizi wa Musa.
Awali katibu wa CCM wilaya ya Njombe Hanafi Msabaha anasema utendaji wa Magufuli umeacha alama kubwa kwani umeweza kujenga miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo barabara,soko lenye hadhi ya kimataifa,hospitali na kituo kikubwa cha mabasi na kwamba wataendelea kumtanguliza mungu na kuchapa kazi .
Baadhi ya wananchi akiwemo Zawadi Muhamed misi utalii mkoa wa Njombe,Rehema Nyenzi na Yared Tweve wanasema maombi yao yatasaidia kumpunguzia adhabu ya kaburi kutoka jitihada zake za kujenga Tanzania.
Katika maombezi hayo pia imetolewa sadaka ambapo kiasi cha zaidi ya laki 2 kimepatikana na kisha kuahidi zinatolewa kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Kibena ili kumsindikiza hayati kwa kutenda matendo ya huruma
Mwili wa hayati Magufuli unahifadhiwa leo katika nyumba milele wilayani Chato mkoani Geita.