Katibu wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara tawi la mererani Rachael Njau akisaini kitabu cha maombolezo ya hayati Rais John Magufuli kilichopo Katina ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
………………………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza, ARUSHA
Kufuatia kifo cha Rais John Magufuli, huduma ya Yesu nuru ya watu imeandaa ibada maalumu ya siku tano kumuombea pumziko la milele na kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu wakati wote wa maombolezo na baada ya maombolezo.
Hayo yameelezwa na nabii utukufu kwa bwana Peter Lais wakati alikiongeza na waandishi wa habari na kusema maombi hayo yameanza jana march 24 katika ukumbi wa metropol na yatafanyika kwa siku tano hadi march 28 ,na kushirikisha wananchi wote wa dini zote na mathehebu yote.
Alisema niya maombi haya ni kumuombea aliyekuwa Rais wa nchi yetu hayati Magufuli ,kumuombea Rais Samia Suluhu ,viongozi wote wa nchi,wananchi pamoja na nchi yetu kwa ujumla .
Alisema umuhimu wa kuombea nchi nikutaka Tanzania iendelee kuwa na amani ,na kusisitiza ni vyema kila mwananchi kusimama kidete na kuiombea nchi yetu kwani hakuna mwananchi anaweza kutenganisha maisha yake na nchi ukiwa kama wewe ni mtanzania.
“Nivyema tukaombea nchi yetu kila mtu kwa dhehebu lake na imani yake maana ili nchi yetu iwe na amani maana amani ya Tanzania ikipotea ,hata wewe mwananchi utapoteza amani ,nashangaa baadhi ya watanzania wanachochea uvunjifu wa amani niseme tu wanakosea sana na wanatakiwa wajitafakari mara mbilimbili kabla hawajaendelea kuchochea uvunjifu wa amani”alisema Peter
Alisema kuwa katika kipindi hichi cha maombolezo kumetokea watu ambao niwakosoaji sana,watu wanaokosoa nchi yetu ,watu ambao wanaokosoa viongozi wetu kuliko watu ambao wanasimama na Mungu kuendelea kuiombea amani ya nchi yetu kitu ambacho kinasikitisha na sio kwa wananchi tu bali ata Mungu mwenyewe hapendezwi na watu hao.
“Nashangaa sana kuona baadhi ya watu wanashangilia kifo cha Rais Nanina diriki kusema wale wote ambao wanashangilia kifo cha hayati Magufuli ni wajinga kwani ni kiongozi ambaye naweza sema alikuwa kuhani au nabii kwani ametufanyia mengi ni kiongozi ambaye aliweza kuwaondolea watanzania hofu na hadi sasa tunaishi ,ameweza kuzuia mengi na pale anapozuia baada ya muda tunasikia matokeo ukiangalia ata chanjo ya ugonjwa wa Covid 19 yeye ndio wa kwanza kukataa watanzania wasichanjwe na baada ya muda hao wazungu walioleta nao wakakataa sasa nikisema mtu anaefurahia kifo cha uyu kiongozi ni mjinga nitakosea ,”alibainisha Peter
Alisema kuwa hiki ni kipindi cha watanzania wote kushikana mikono kwa pamoja ,aliwataka watanzania kutoruhusu mapengo yoyote , kitu chochote au mtu yeyote yule atutenganishe ,na kubainisha kuwa huu ni wakati wa kusimama na Mungu kuombea nchi pamoja na kushikamana kwani iwapo amani ya nchi itaparanganika ata wananchi pia wataparanganika .
Alibainisha kuwa watu wengi wameguswa na msiba wa hayati Rais John Pombe Magufuli, amefanya mambo mengi kwenye sekta ya afya ambapo ameweza kujenga hospitali katika kila wilaya ,sekta ya elimu ameweza kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, maji kwa mkoa wa Arusha ameweza kuwapa mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520 barabara, usafiri wa anga ameleta ndege,treni ,umeme alipoingia madarakani alikuta vijiji 2000 tu vinaumeme sasa zaidi ya 9000 vimewekwa umeme hivyo wananchi wameguswa na maendeleo yaliyofanywa nae.
Aliwataka wananchi waendelee kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kuweza kwenda na kasi aliyokuwa akienda nayo hayati ya kuwaletea watanzania Maendeleo