Home Michezo NDOTO YA TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2022 YAZIMWA NA EQUATORIAL GUINEA

NDOTO YA TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2022 YAZIMWA NA EQUATORIAL GUINEA

0

TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Equatorial Guinea jana Uwanja wa Nuevo do Malabo.
Katika mchezo huo wa Kundi D kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani Cameroon, bao pekee la Equatorial Guinea lilifungwa na Nahodha wake, Emilio Nsue Lopez dakika ya 90.
Sasa Equatorial Guinea inafikisha pointi tisa na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Tunisia zote zikifuzu AFCON ya mwakani. 
Tanzania inabaki nafasi ya tatu na itamenyana na Libya wiki ijayo Dar es Salaam kukamilisha ratiba.